MWANAMAMA mkali kwenye Tamthiliya za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amefunguka kuwa, katika kipindi cha sasa, mambo ya maonesho yamepitwa na wakati kwani lazima kila mtu ajue kushughulika na vitu vya maana na vya kumjenga.
Batuli ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, nyakati zimebadilika na wakati wa sasa siyo wa kuoneshana mtu amenunua gari gani au amevaa nguo ya bei ghali kiasi gani, badala yake ni wakati wa kuangalia ni kitu gani cha kufanya kwa ajili ya maendeleo.
“Mara nyingi hata mimi nakuwa sionekani hovyohovyo kwa sababu huu siyo wakati wa maonesho. Sasa hivi ni kupiga kazi na kujua kipi ufanye ili ujiletee maendeleo binafsi na siyo kujionesha,” anasema Batuli.