Beyonce kuachia albamu yake mpya ya 'Black is King' mwezi huu



Mwanamuziki wa nchini Marekani, Beyonce Knowles ameachia kionjo cha ujio wa Albamu yake mpya ya Black Is King atakayoiachia mwishoni mwa mwezi huu. 

Album hii mpya Black Is King itahusisha nyimbo mbalimbali zilizokuwepo kwenye mfululizo wa ngoma zilizozalishwa kwenye filamu ya 'The Lion King' inayotimiza mwaka mmoja mwezi huu. 

Aidha, Albamu hiyo inatarajiwa kuachiwa kupitia Disneyplus ambapo itatoka kwa mfumo wa televisheni na mtandao. 

Hii itakuwa mara ya pili kwa Beyonce kuachia Albamu yenye kutoka kwenye mfumo wa mtandao na televisheni baada ya #HomeComing mwaka 2019. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad