Mtanzania Saniniu Kuryan Laizer ambaye hivi karibuni aligeuka kuwa bilionea baada ya kupate mawe ya madini ya Tanzanite yenye thamani ya shiling bilioni 7.8, ameagundua jiwe lingine la Tanzanite lenye thamani ya mabilioni kwa shilingi za kitanzania.
Jiwe hilo lina uzito wa kilo 6.33, na thamani yake kamili inatarajiwa kutangazwa rasmi baada ya kuthamanishwa kwa jiwe hilo. Jiwe la sasa alilolipata Saniniu Kuryan Laizer ambaye ni mchimbaji madini mdogo linasemekana kuwa ni jiwe la pili kwa ukubwa kuwahi kupatikana katika machimbo ya madini hayo kaskazini mwa milima ya Mirelani .
Mwezi mmoja tu uliopita alipata madini ambayo moja lilikua na kilo 9.2 likiwa na thamani ya bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani ya shilingi bilioni 3.3. Serikali inatarajiwa kukabidhiwa jiwe la hivi karibuni kutoka kwa Bwana Laizer ambapo inatarajiwa kuwa atakabidhiwa pesa kutokana na jiwe hilo.
Saniniu Kuryan Laizer mwenye umri wa miaka 52, ni mume wa wanawake wanne na amejaliwa watoto 30.