Bodi ya Mikopo Yaja na Mpya Kwa Wanufaika
0
July 29, 2020
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB), imesema kuwa uwepo wa vitambulisho vya Taifa, utasaidia bodi hiyo katika kuwabana wanufaika wa mikopo ili waweze kurejesha kwa wakati.
Mkuu wa Mawasiliano ya Bodi hiyo, Omega Ngole amesema kuwa wanaufaika wengi wamekuwa wakijificha pindi wanapohitimu elimu hiyo ya juu, hivyo kuisababishia hasara bodi na kupelekea wanafunzi wengi kukosa mikopo.
Aidha Omega ameongeza kuwa makato hayo ya asilimia 15 yanayopingwa na baadhi ya wadau nchini, yamefanya bodi ikusanye marejesho ya Shilingi Bilioni 18.9 ndani ya mwezi mmoja.
Tags