Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, ameshangaa kitendo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Vincet Mashinji, kupata kura mbili kwenye uchaguzi wa kura za maoni kuwania ubunge jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam.
Boniface ametuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter huku akihoji kuwa kitendo cha kutoka ukatibu Mkuu wa Chama cha upinzani hadi kupata kura mbili maana yake nini.
“Kwako mwalimu Kashasha hii ya huko Kawe, mtu kutoka kuwa katibu mkuu wa chama cha kikuu cha upinzani mpaka kupata kura 02 maana yake nini? a) CCM haipendi Wasaliti? b) CCM Kawe wanajua lile Kopo tupu Kichwani? c) CCM Kawe haitaki watu wenye tamaa tamaa ya ovyo?” Alihoji Jacob.
Jimbo la Kawe walijitokeza wagombea 170 katika uchaguzi uliofanyika leo Mashinji alitangazwa kupata kura mbili huku mshindi wa kwanza akiwa ni Furaha Dominc aliyeibuka kidedea kwa kura 101.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, aliambulia kura 79 na kushika nafasi ya tatu na mshindi wa pili ikichukuliwa na Angela Kizinga kwa kupata kura 85
Kwako Mwalimu Kashasha @IAMartin_— Boniface Jacob (@MayorUbungo) July 21, 2020
Hii ya huko Kawe,Mtu kutoka Kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikuu cha Upinzani Mpaka Kupata Kura 02 Maana yake Nini?
a)CCM haipendi Wasaliti?
b) CCM Kawe Wanajua lile Kopo tupu Kichwani?
c)CCM kawe haitaki Watu Wenye tamaa tamaa ya ovyo?