CCM Kawe wamkataa Gwajima Ubunge, Wasema Yakaidhari Mpe Kaidhari
0
July 22, 2020
Wajumbe wa CCM waliopiga kura ngazi ya jimbo Kawe, wamemchagua Furaha Dominic Jacob kuwa mgombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo kwa kura 101.
Mchungaji Josephat Gwajima ambaye alionekana kuwa moja ya washindani wenye nguvu kwenye jimbo hilo ameshika nafasi ya tatu kwa kura 79 huku nafasi ya pili ikishikwa na Angella Charles Kiziga kwa kura 85.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na baadaye kuhamia CCM, Vincent Mashinji amefanikiwa kupata kura 2 kati ya kura 475.
Aidha, aliyewahi kuiwakilisha CCM katika Jimbo hilo mwaka 2015, Kippi Warioba amejikusanyia kura 3 katika Mkutano huo.
Tags