Chadema yapanga Kumpokea lissu, Jeshi la Polisi Laonya



Jeshi la Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kuhamasisha wananchi kukusanyika kinyume cha sheria na hivyo kuagiza kuacha mara moja tabia hiyo la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


Hatua hiyo inakuja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza siku ya kwenda kumpokea Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya chama hicho, Tundu Lissu ambaye amekuwa nje ya nchi tangu Septemba 7, 2017 anayetarajiwa kurudi nchini Julai 27  mwaka huu.


Msemaji wa Jeshi hilo, SACP David Misime amesema wamefuatilia nchi nzima kuona kama kuna taarifa iliyofikishwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya mkusanyiko huo lakini hawakukuta taarifa yoyote.


“Tumeona katika mitandao ya kijamii baadhi ya viongozi wa Chadema wakihamasisha wananchi kukusanyika kutoka maeneo mbalimbali ya nchi Julai 27, ili kumpokea kiongozi mmoja wa chama hicho anayetarajiwa kurejea nchini.


“Kurejea   kwake ni haki yake kama ilivyo kwa Watanzania wengine kwasababu nchi yetu iko salama sana kwa maisha ya Watanzania hata kwa wageni wanaofika nchini na kukusanyika ni haki ya kila Mtanzania lakini hakuna haki isiyokuwa na wajibu kwa mujibu wa sheria za nchi,” amesema SACP Misime.


Jeshi hilo pia limetoa wito kwa wanafunzi wenye nia ya kugoma na kutoingia darasani kwa madai ya kuishinikiza Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kurejea masharti ya mkopo kati ya serikali na mwanafunzi wa fedha za kujikimu na hiyo kuagiza kutoshiriki kitendo hicho na badala yake wafuate sheria, kanuni na taratibu ya kutatua jambo hilo badala ya kufuata taratibu ambazo hazina Baraka za kisheria wa miongozo ya vyuo vikuu.


“Hivi sasa tunashughulika na jambo moja kubwa la kuomboleza kifo cha Rais wetu mstaafu, Benjamin Willium Mkapa na Watanzania hawategemei kuona mtu yeyote anakosa busara na kuanzisha mambo mengine yaliyo kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi,” amesema SACP Misime.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad