Chura wa kipekee aliyesafiri kisiri kwa ndege kutoka Marekani apatikana Uingereza



Chura wa kipekee aliyesafiri kisiri ‘stowaway’ ameishia kwenye duka kubwa la kufanya manunuzi baada ya kusafiri maili 5,000 kutoka Amerika Kusini.

Mfanyakazi mmoja wa duka la Llanelli ndiye aliyembaini chura huyo katikati ya ndizi zilizokuwa zimewasilishwa kuuzwa kwa wateja.

Inasemekana kwamba chura huyo aliyepewa jina la Asda aliwasili kutoka Colombia ambapo mamia na maelfu ya tani za ndizi huzalishwa na kupelekwa Uingereza kila mwaka.

Sasa hivi chura huyo anatunzwa na watalaamu huko Pembrokeshire ambako anakula nyenje na nzi, timu ya uokozi imesema.

Timu ya hiyo ilifahamishwa kuhusu chura huyo baada ya mfanyakazi mmoja gundua uwepo wake akiwa kazini.

Wanyama aina ya amfibia wana uwezo wa kupunguza kasi ya mmeng’enyo wa chakula katika mazingira tofauti na hiyo ndio inasemekana kuwa njia moja iliyomwezesha chura huyo kunusurika kifo licha ya safari ndefu bila chakula wala maji hadi eneo ambalo hali ya hewa ni baridi.

Hifadhi ya wanyama wa baharini yashukuru wafanyakazi wa Asda kwa kumbaini chura na kumtunza hadi alipookolewa cha kituo hicho
Chura Asda kwa sasa hivi amehamishwa hadi hifadhi ya wanyama ya ‘Silent World Zoo To You’ kituo maalum cha wanyama wa baharini huko Haverfordwest ambako sasa atakuwa anaishi katika maeneo ya mazingira ya mimea, na unyevuunyevu.

Wafanyakazi katika hifadhi aliyopelekwa chura huyo wanaamini kwamba ni aina ya wanaoishi mazingira ya mimea.

“Chura huyu wa kipekee amesafiri maili 5,000 akiwa kwenye mikungu ya ndizi, kutoka eneo lake la asili Colombia hadi duka la manunuzi la Llanelli, amesema mkaguzi wa duka hilo, Gemma Cooper.

“Bila shaka ni safari ndefu.”

‘Asda’sasa hivi yuko kwenyehifadhi ya wanyama wa baharini kituo cha Pembrokeshire
Bi. Cooper ameshukuru wafanyakazi wa duka la Asda kwa kumbaini na kumtunza chura huyo hadi alipookolewa.

“Kwa matunda yanayosafirishwa nje ya nchi jinsi yanavyopulizwa dawa na kutunzwa sio kawaida kuona chura au buibui akisafiri kwa kujibanza kwenye matunda hadi eneo lililokususdiwa,” amesema.

“Kwa bahati nzuri anaendelea vyema na zaidi aliweza kwendana kabisa na mazingira ya mmea wa mgomba wakati tunamsaidia kuanza kuzoea makazi yake mapya.

Je hawa ni vyura wa aina gani?
Kuna takriban vyura 800 wa aina hii huku zaidi ya 600 wakiishi Amerika ya Kati na Kusini.
Vyura hawa wanapatikana kwa rangi tofauti tofauti na baadhi hubadilika rangi ili kwendana na mazingira kama kinyonga
Wengi wao huwa wadogo kiasi cha kuweza kuketi vizuri tu kwenye kidole kimoja cha mwanadamu
Pia wanatumia macho yao kuwasaidia kula chakula. Wanafunga macho yao kabisa ili kuweza kusukuma chakula kipite kooni
Baadhi, ngozi yao inatumiwa na watu wa asili kutengeneza dawa za kulevya.
Chanzo: BBC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad