Wahenga walisema ukiona wingu zito limetanda angani ujue kuna mvua kubwa inakuja kunyesha hivyo chukua tahadhari na tafuta mahala salama ujikinge. Siku zinazidi kuyoyoma na wapinzani wa CCM ndio wanazidi kunywea maana wanajua kwenye uchaguzi wanaenda kukutana na kichapo cha ukweli.
Ninajua wanajiuliza majukwaani watanadi sera gani? Wanakosa majibu. Wanajiuliza tukisimamisha wagombea wa ubunge wanakosa majibu nani atafaaa au nani atarudi tena. Wamekuwa wa baridi na hatusikii hata dalili za watia nia wao maana kila jimbo ni kama kuna shoti ya umeme na wanaogopa kuweka mkono.
Lakini nini hasa sababu ya haya yote? Ni uadilifu, uchapakazi na uzalendo wa JPM ndio umeipa nguvu na kiburi CCM na sasa ina uhakika wa kuchukua kiti cha ubunge au udiwani katika eneo lolote. Maana ni ndani ya miaka minne tu, watu wameshuhudia mabadiliko makubwa sana.
Sekta ya afya, elimu, miundombinu na ulinzi na usalama zote zimeimalishwa. Wapinzani uchwara wanaona aibu tu kukubali na kukaa kando. Lakini wangekuwa na busara wangetulia na kukaa kando.
Wameishiwa tena ile Mbaya. Walikuwa wanaitumia Saccozi ili wawadhulumu na Kuwanyonya wabunge na Wanachama. sera kuch nehi.
ReplyDeleteCha kuuza kwa wananchi Hawana... FARU JONI MTINDO MMOJA..!!