Dawa ya HIV imepatikana? Wanasayansi waonya kuhusu kusherehekea mapema baada ya jamaa mmoja kudaiwa kupona HIV Brazil
0
July 09, 2020
Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 36 nchini Brazil huenda akawa mtu wa kwanza kupona HIV bada ya kutubiwa kwa mseto wa dawa za kukabiliana na virusi hivyo ,watafiti wamesema .
Ni watu wawili pekee ambao wamethibitishwa kupona ugonjwa huo baada ya matibabu yanayofanywa kwa njia ya kitaalam na hatari sana yalihusisha kuondolewa kwa ‘Bone marrow’ kutibu kansa zinazozuka baada ya ugonjwa huo kukithiri mwilini .
Mgonjwa huyo Brazil hajaonyesha daalili za maambukizi ya HIV baada ya kufanyiwa vipimo vya damu kulingana na watafiti katika chuo kiku cha Sao Paulo kinachotambulika kwa tafiti za hali ya juu .
Wamesema kisa hicho ni cha mwanzo na majaribio ,huenda ndicho cha kwanza kwa matibabu ya kudumu ya mtu aliyeambukizwa HIV .
Lakini katika mataifa mengine watafiti wametaka pawepo tahadhari katika kuanza kutangaza ushindi wa mapema dhidi ya HIV . Dr Steve Deeks ambaye ni mtafiti wa HIV kutoka chuo kikuu cha California amesema ukosefu wa antibodies katika mgonjwa huyo ni jambo la kushangaza katika kisa hicho na utafiti zaidi unafaa kufanywa kubaini hali hiyo ndiposa pawepo uhakiki wa kupatikana kwa tiba ya kudumu ya HIV .
Deek amesema ni mapema sana kujua iwapo mgonjwa huyo wa Brazil ana ukimwi hadi matokeo hayo yathibitishwe na maabara huru
Tags