DC Musoma Kufunga Shule kwa Kukithiri Vitendo vya Kishirikina
0
July 19, 2020
Mkuu wa wilaya ya Musoma, Vicent Naano ametoa wiki moja kwa Wananchi wa Kijiji cha Kakisheri wanaojihusisha na matukio ya kishirikina kuacha vitendo hivyo haraka na endapo vitandelea basi atafunga shule ya msingi Kambarage na kuwahamisha Walimu.
DC huyo ametoa agizo lenye onyo kwakuwa Shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na matukio yasiyo ya kawaida ikiwemo Walimu kuingiliwa kimwili nyakati za usiku, kulazwa nje na wanafunzi kudondoka hovyo na kupiga kelele.
Imeelezwa kuwa matukio ya wanafunzi wa darasa la 7 kuanguka na kupiga kelele, kukuta chakula aina ya makande kikiwa kimewekwa chooni yaliwalazimu walimu, wazazi na wanafunzi kupiga kura ili kubaini anayefanya matukio hayo kwa imani ya kishirikina.
Tags