Dkt. Mwakyembe Atekeleza Agizo la JPM Kuhusu COSOTA




KUFUATIA agizo la Rais Dk. Magufuli la kutaka Chama cha Haki Miliki Tanzania (COSOTA) kuhamishwa kutoka katika Wizara ya Viwanda na Biashara na kuhamishiwa katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo limeanzwa kutekelezwa rasmi leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe amesema amepokea kwa furaha uamuzi huo wa Rais kwani umelenga kukuza na kuboresha maslahi ya wasanii nchini kutokana na shughuli zao za kisanaa.

Dkt. Mwakyembe amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma. Hata hivyo, Mwakyembe ameweka wazi kuwa Rais Magufuli tayari ameshasaini waraka wa kuihamisha COSOTA kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na kuhamia katika Wizara anayoisimamia yeye.

Aidha, Waziri Mwakyembe amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni na Sanaa, Dk Hassan Abbas kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara ndani ya saa 24 kwa ajili ya kupeana makabidhiano pamoja na kutembelea Ofisi za COSOTA na kukutana na wadau wote wa Sanaa.

“Niwatake wenzangu ndani ya Wizara yetu kutambua kuwa tuna jukumu kubwa sana kulinda imani ya Rais wetu kwa kutuamini na kutupa fursa ya kumsaidia kusimamia kazi na hati miliki za wasanii ambao yeye anawaamini na kuwapenda,” amesema Dk Mwakyembe.

Dk Mwakyembe amesema mara baada ya agizo la Rais Magufuli tayari Wizara hiyo imeanza kukaa vikao kwa ajili ya kujipanga kuangalia namna ya kuipokea COSOTA pamoja na kuweka utaratibu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad