Emmanuel Mbasha autaka Ubunge,achukua fomu Singida



Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Tanzania Emmanuel Mbasha amonyesha nia ya kuutaka Ubunge baada ya leo hii kuchukua fomu ya kugombea katika Jimbo la Iramba Mashariki Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida

Akitangaza nia hiyo kwenye picha na ujumbe aliouweka kwenye mtandao wa Instagram Emmanuel Mbasha ameandika kuwa

" Mungu kama uishivyo nakuomba nibariki safari yangu hii mpya ya kuwatumikia wananchi wa Mkalama, nimechukua fomu kugombea Ubunge Jimbo la Iramba Mashariki, Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida, naomba maombi yenu rafiki zangu wote, Mungu ibariki Tanzania"

Mpaka sasa sura mpya zilizotangaza nia ya kugombania Ubunge ni Wakazi, Master J, Mc Pilipili, Lilian Kamazima, Zamaradi Mketema, Dr Cheni, Kingwendu, Steve Nyerere na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad