Falsafa ya Pesa inayowatofautisha Watu Maskini na Matajiri
0
July 23, 2020
Ili kufanikiwa kifedha, ipo falsafa ya mafanikio ambayo inatumika kuwaongoza watu na hadi kufikia mafanikio hayo makubwa sana ya kifedha. Falsafa hiyo ndiyo inayopelekea wengine wakawa na pesa na wengine wakawa hawana, wengine wakawa matajiri na wengine wakawa maskini.
Kwa mfano, falsafa kubwa ya watu wenye mafanikio hasa linapokuja suala la pesa, ukilinganisha na wale ambao hawajafanikiwa iko hivi; watu wenye mafanikio falsafa yao ipo kwenye kuwekeza kila aina ya pesa wanayoipata hata iwe ndogo vipi. Na kile kiasi kidogo kinachobakia hukitumia katika katika matumizi ya kawaida, lakini mara baada ya kuwekeza.
Wakati watu ambao hawajafanikiwa nao pia falsafa yao ya pesa ni kutumia kila pesa wanayoipata na kiasi kidogo kinachobakia hicho ndio huanza kujaribu kuwekeza. Watu wasio na mafanikio, matumizi ndio kipaumbele cha kwanza kabisa kabla ya uwekezaji wowote ule.
Bila kujali shida zetu tulizonazo, changamoto mbalimbali, Ili kufanikiwa unatakiwa kujiwekea falsafa ya pesa kama wanavyofanya matajiri, ni lazima uanze kuwekeza kwanza hata kwa pesa kidogo, halafu matumizi yatafuata, kinyume cha hapo utakwama sana na utashindwa kufikia uhuru wa kipesa.
Je, unavyofikiri kwa falsafa hizo mbili, je, hali ya maisha inaweza ikawa sawa kwa watu hao wawili kutokana na matumizi ya hizo falsafa? Najua majibu mpaka hapo unayo kwamba falsafa ipi ni sahihi. Kama utatumia falsafa ya pesa ya watu wasiofanikiwa, tambua utakuwa hivyo na ukitumia falsafa ya pesa ya watu wenye mafanikio, utafanikiwa pia.
Na. Imani Ngwangwalu
Tags