Rais Magufuli apingwa Mahakamani,Wakili Fatma Karume aongoza ...Aliyekuwa Rais wa chama cha mawakili cha Tanganyika (TLS) Fatma Karume amehoji ni kwa nini Rais John Magufuli asiwe rais wa maisha yote nchini baada ya hoja ya kumuongezea kipindi cha miaka miwili zaidi ya kutawala.
Karume ametoa kauli hiyo alipokuwa anajibu juu ya hoja iliyoanzishwa kwenye mtandao wa twitter juu ya rais Magufuli kuongezewa miaka miwili baada ya kumaliza awamu yake ya uongozi.
“Huu WITO wa kuongeza muda Magufuli kama SHUKRANI ina msingi DHAIFU na POTOFU lakini tusema tunakubali kudharau hilo, Swali langu: 1 Kwanini tumuongozee miaka 2 tu? 2.Nani kapima urefu wa SHUKRANI yetu akafikia miaka 2? 3. Kwanini asiwe PRESIDENT FOR LIFE?, Tutafakari kabla kusema” ameandika Karume kwenye ujumbe wake kwenye ukurasa wa twitter.
Rais Magufuli amekuwa akisisitiza mara kadhaa kuwa hataki kuongeza hata dakika moja kwenye nafasi ya urais kutokana na ugumu wa kazi hiyo.
Huu WITO wa kuongeza muda Magufuli kama SHUKRANI ina msingi DHAIFU na POTOFU lakini tusema tunakubali kudharau hilo, Swali langu:— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) July 13, 2020
1 Kwanini tumuongozee miaka 2 tu?
2.Nani kapima urefu wa SHUKRANI yetu akafikia miaka 2? 3. Kwanini asiwe PRESIDENT FOR LIFE?
Tutafakari kabla kusema https://t.co/wTzC3gf5Na
goodness
ReplyDelete