Fei Toto Akabidhiwa Tuzo & Mil 1 na SportPesa
0
July 30, 2020
Mchezaji wa timu ya Yanga Feisal Salum (Feitoto) akikabidhiwa tunzo ya ushindi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas baada ya kuibuka bingwa kwenye shindano lililoendeshwa na wadhamini wakuu(SportPesa) kwa mchezaji bora wa timu ya Yanga kwa msimu 2019/2020 wa ligi kuu Tanzania Bara.
KAMPUNI ya michezo na burudani ambao pia ni wadhamini wakuu wa timu za Simba na Yanga wiki hii waliendesha shindano la kumpata mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara kwa timu wanazozidhamini.
Kwa upande wa Yanga mshindi aliibuka Feisal Salum na kwa upande wa Simba mshindi aliibuka Clatous Chama.
Shindano hili liliwataka mashabiki wa timu hizi mbili kumpigia kura mchezaji wao bora na aliyefanya vizuri kuanzia mwanzo wa ligi mpaka hitimisho kupitia mitandao wa kijamii ambapo mshindi atakabidhiwa tunzo kama
ishara ya ushindi na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 1.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa Feitoto alisema “Kwanza kabisa napenda kuwashukuru sana sana wadhamini wetu SportPesa kwa kutukumbuka sisi wachezaji na kutambua zaidi vipaji vyetu kwani hii inatupa motisha ya kufanya vizuri zaidi na zaidi.”
“Pili niwashukuru mashabiki wa Young Africans kwa kunipigia kura kwa wingi na kuhakikisha naibuka mshindi kwa timu yangu.” “Pia napenda kuushukuru uongozi mzima wa Yanga kwa nafasi waliyonipa,kuniamini kama mchezaji wao.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas wakati wa mkutano na waandishi wa habari maalum kwa kukabidhi tuzo hiyo alisema “Safari hii tumewapa nafasi wachezaji waweze kupendekeza na kumuwezesha mchezaji wa timu yao pendwa kushinda kwa kumpigia kura mara nyingi wawezavyo ili kushinda zawadi hizi”.
“Hii ni mara ya kwanza kwa SportPesa kutoa tunzo hizi kwa mchezaji wao bora ikiwa na lengo la kuwahamasisha na kuongeza ushindani mkubwa baina yao ambao utapelekea kwa timu nzima kuendelea kufanya vizuri
zaidi na zaidi kwenye michuano ijayo.
“Nawashukuru sana mashabiki wa timu zote mbili kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa hasa kuhakikisha wanawapigia kwa wingi wachezaji wao hadi kuibuka washindi.
Msemaji mkuu na muhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz naye alimaliza kwa kusema “msimu huu haukuwa mzuri kwetu lakini ningependa kuwaomba mashabiki waendelee kutuonyesha ushirikiano na waendelee
kutamba kwani yajayo yanafurahisha.
Tags