Google Yatuhumiwa Kuingilia Faragha za Watumiaji
0
July 15, 2020
Google na kampuni yake Mama iitwayo Alphabet Inc wameshtakiwa kwa kuingilia faragha za mamilioni ya watumiaji wake kinyume na utaratibu na kutakiwa kulipa fidia ya dola bilioni 5
Walalamikaji wanasema Google imekuwa ikikusanya taarifa za watumiaji wakiwa 'online', kujua wanatafuta nini, taarifa gani wanafuatilia na wanafanya nini kwenye 'App' zao hata wakiwa kwenye 'private mode'
Aidha, shtaka linaeleza kuwa hata pale wateja wanapofuata maelekezo na kuzima nyenzo zote za kufuatiliwa bado Google huendelea kufuatilia na kuingilia shughuli zote zinazofanywa na wateja wake katika wavuti mbalimbali
Ukusanyaji wa data hizo husaidia Google kujua maisha ya faragha ya kila mtu mwenye simu au kompyuta ikiwemo kujua marafiki zao ni akina nani?, wanapenda kula nini?, kununua nini?, na hata kujua vile vitu vya aibu mtu alitafuta 'online'
Hadi sasa bado Google hawajatoa maelezo yoyote kufuatia tuhuma hizo.
Tags