GSM Yafunga Hesabu, Hivi Hapa Vifaa Vipya Yanga



WADHAMINI wa Yanga, Kampuni ya GSM rasmi imewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa kila kitu kuhusu usajili wao umekamilika na jumla ya washambuliaji wawili, winga na mabeki wa pembeni na kati watatua Agosti Mosi, mwaka huu.

Kauli hiyo hiyo ya kibabe ameitoa Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said ambaye yeye ndiye alikabidhiwa fungu la fedha kwa ajili ya kukamilisha usajili wa nyota hao watakaotua kuichezea timu hiyo kuelekea msimu ujao.


GSM hivi karibuni ilijiapiza kufanya usajili wa kisasa na bora utakaoendana na hadhi ya klabu yao huku ikitoa ahadi ya kubeba mataji yote ya ubingwa mara baada ya kuchukua timu hiyo katika kuelekea msimu ujao.

Akizungumza na Championi Jumamosi,Hersia lisema kuwa wamepanga kusajili wachezaji tisa pekee katika kuelekea msimu ujao kati ya hao watano wa kimataifa ambao mastraika wawili, winga, kiungo mkabaji na beki wa kushoto.

 
Hersi alisema kuwa wachezaji hao wataanza kutua Agosti Mosi mara baada ya ligi kumalizika baada ya kumalizana nao, kati ya hao wapo wanaotajwa kwenye vyombo vya habari na wasiotajwa ambao ni washambuliaji Heritier Makambo (Horoya AC), Jese Were, Maric Makwata (wote Zesco ya Zambia) kati ya wawili hao mmoja ndiye atakayetua mara baada ya klabu inayowamiliki itakapokubali kumuachia.

Wengine ni Sogne Yacouba, Michael Sarpong (wote huru), winga Tuisila Kisinda (AS Vita), kiungo mkabaji Ally Niyonzima na Eric Rutanga (Rayon Sports), huku wazawa wanaotajwa ni mabeki wa pembeni Yassin Moustapha (Polisi Tanzania), Kibwana Shomari (Mtibwa) na beki wa kati Haji Shaibu ‘Ninja’.

Mtoa taarifa huyo aliongeza kuwa, wachezaji hao watatua nchini haraka kwa ajili ya kusaini mikataba sambamba na kuingia kambini kujiandaa na msimu ujao.

“Hatutavunja kambi kama tulivyotangaza awali, kwani timu itaendelea na kambi ya kujiandaa na msimu ujao lengo ni kuwa na ‘pre-season’ ndefu kwa ajili ya wachezaji wetu kupata muda wa kuzoeana ili kabla ya ligi timu imejengeka kwa maana ya kucheza kitimu.

“Kwani tumepanga kufagia kwa kuwaondoa wachezaji wasiokuwepo kwenye mipango yetu baada ya kocha kutoa ripoti yake ya usajili kwa wachezaji asiowahitaji, hivyo wale asiowataka tutavunja mikataba yao kwa kulipa stahiki zao ili waondoke kwa heri.

“Upo uwezekano mkubwa wa kikosi chetu cha kwanza cha msimu ujao kuwepo na wachezaji na wachezaji watatu hadi wawili pekee na wengine wote watakuwa wapya, hivyo lazima timu ikae pamoja ili kocha apate muda wa kukiandaa kikosi chake,” alisema Hersi.

Stori: Wilbert Molandi na Musa Mateja
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad