Habari Njema kuhusu Covid19 Afrika, Chanjo Kuwasili
0
July 10, 2020
Bara la Afrika huenda likanasua kutokana na minyororo ya janga la virusi vya corona mapema 2021 iwapo majaribio yanayofanyiwa chanjo Afrika Kusini yatazaa matunda.
Shabir Madhi, profesa wa Oxford ambaye yuko katika mstari wa mbele katika kufuatilia majaribio hayo ameeleza kuwa chanjo hiyo huenda itakuwa tayari sokoni mwaka ujao baada ya majaribio yake kukamilika.
Majaribio hayo ambayo yamefanyiwa idadi ya watu 2000 kati ya umri wa miaka 18-65 inatarajiwa kuwa chini uangalizi kwa mwezi 12 kabla kuzinduliwa rasmi kwa matumizi.
Aidha Profesa huyu ameeleza kuwa matokeo ya majaribio hayo huenda yatatolewa kati ya Novemba na Disemba.
Kando na hivyo, Shabir ameeleza kuwa chanjo hiyo itatumika kwa wagonjwa wa 42 wa covid19 na kuwa chini ya uangalizi kwa mwezi mmoja.
Ameeleza kuwa iwapo chanjo hiyo itakuthibitishwa kuwa shawi, tatizo kuu litakuwa kutoa dawa za kutosha kwa umma.
Kwa upande mwingine, shirika la afya ulimwenguni WHO limeyashauri mataifa kuimarisha sekta za afya ili kuwa tayari kwa chanjo kutoka Oxford ambayo pia inatarajiwa Disemba.
Chanjo hiyo ya Oxford ni kati ya maribio 17 ambayo yameonyesha dalili ya kuweza kupita mtihani wa kupombana na virusi vya corona.
Kila nchi iko mbioni kufanya kila iwezalo kupambana na virusi hatari vya corona ambavyo vimeyumbisha uchumi kote duniani.
Tags