Helkopta ya Israel hapo jana imeripotiwa kufanya mashambulizi katika vituo vya kijeshi vya Syria katika mji wa Quineitra huko kusini-magharibi mwa Syria na kusababisha wanajeshi wawili wa Syria kujeruhiwa.
Televisheni ya serikali ya Syria ikinukuu chanzo cha kijeshi imesema helkopta hiyo ilivilenga vituo vitatu katika kipindi kifupi kabla ya usiku wa manane.
Aidha kituo hicho kiliongeza kusema mashambulizi hayo pia yalisababisha kuwaka mtoto kwa maeneo kadhaa katika maeno hayo.
Lakini jeshi la Israel lilisema lilikuwa likiimarisha ulinzi katika eneo la mpaka wake wa kaskazini, katika kipindi hiki ambacho mvutano unaongezea na wapiganaji wa Hezbollah.
Iran imekuwa mshirika mkubwa wa Rais Bashir al-Assad wa Syria tangu kuzuka kwa vuguvugu la kupigania demokrasia dhidi ya utawala wake mwaka 2011.
OPEN IN BROWSER