Hofu ya Uwekezaji Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba
0
July 20, 2020
Wadau na wafanyabiashara waliowekeza katika masoko ya mitaji na dhamana wameondolewa hofu kuhusiana na mwenendo wa masoko hayo katika kuelekea msimu wa uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Wadau na wafanyabiashara waliowekeza katika masoko ya mitaji na dhamana wameondolewa hofu kuhusiana na mwenendo wa masoko hayo katika kuelekea msimu wa uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika mahojiano na EATV iliyotaka kufahamu athari za msimu huo katika uwekezaji Meneja Miradi na Maendeleo DSE Leonard Kameta amesema katika uzoefu wa vipindi vilivyopita ikiwemo msimu wa janga la Covid-19 athari zake zimeendelea kuwa chanya.
Amesema kutokana na usimamizi bora uliofanywa na Rais Dkt. John Magufuli katika sekta mbalimbali bado wawekezaji wa ndani na nje umeendelea kuwa imara wa biashara Tanzania na kuwahimiza wafanyabiashara kuweka mikakati bora ili kukua kiuchumi na kuongeza mapato.
“Serikali imefanya jitihada kubwa kama tulivyoona kipindi cha Corona kutofunga maeneo ya biashara na kutozuia mikusanyiko suala hilo limeleta athari chanya katika uchumi wa nchi ukilinganisha na mataifa mengine,imani yangu hata kipindi cha uchaguzi uchumi utaendelea kuimarika” alisisitiza Kameta
Tags