Huu Hapa Wasifu wa Sumbula wa Tamthilia ya Sultan. Nimekuwekea kwa Lugha Adhimu ya Kiswahili

Sumbula ni Character iliyojipatia umaarufu mkubwa miongoni mwa watazamaji wa tamthilia ya Sultan nchini tanzania.

Tamthilia hii huonyeshwa kwenye King'amuzi cha AzamTv kupitia chaneli yao ya Azam Two.

Jina lake ni Selim Bayraktar, amezaliwa mwezi wa saba mwaka 1975 katika mji wa Kirkuk nchini Iraq.

Alianza kutambulika rasmi katika Tasnia ya uigizaji wa mwaka 2006 alipoigiza kama Erdal katika Tamthilia ya kituruki iliyofahamika kwa jina la "Kopru".

alizaliwa katika Familia yenye mchanganyiko wa ki-Iraq na Kituruki na alipokuwa kijana alianza kujihusisha na mashindano ya michezo ya viungo.

Katikati ya miaka ya themanini ambapo vita vya iran na iraq vilikuwa vinafikia ukingoni, aliyekuwa rais wa nchi hiyo Sadam Hussein, alituma mawakala wake waende wakatembelee shule aliyokuwa anasoma Selim kwa lengo la kuchagua vijana wakakamavu watakao jiunga na Jeshi.

Selim alibahatika kuwa mmoja ya vijana waliofaulu kuteuliwa kujiunga na Jeshi la iraq lakini Familia yake haikupendzwa. hivyo wakaamua kumtoroshea nchini Uturuki.

Nchini Uturuki alijunga katika chuo mashuhuri kinachofamika kama Hacettepe University.

Baada ya kumaliza masomo yake ya chuo kikuu mwaka 2000, akaanza kufanya kazi katika Theatre kuu ya Taifa nchini humo sambamba na kushiriki katika ziara mbalimbali za sanaa za majukwaani ndani na nje ya Uturuki.

Kuhusu uigizaji, Selim Bayraktar ameigiza katika Filamu na tamthilia nyingi. Tamthilia zilizompatia umaarufu ni Kopru ,Bir Bulut Oslam, MuhteÅŸem Yuzyil(Sultan) na Coban Yildizi iliyotoka rasmi mwaka 2017.

Kando na uigizaji, Selim Bayraktar ana uwezo wa kuzungumza Lugha nne: Kituruki, Ottoman-Kituruki, Kiarabu na Kikurdi.

Naam huyu ndio Selim Bayraktar almarufu Sumbula.

Ruksa ku-share ila tafadhali usisahau kumtaja au kumtambua muandishi wa makala hii fupi ambaye ni mimi jamvini storyteller . Nitakushukuru kwa uungwana wako.

Nimeiandika kwa msaada wa vyanzo mbalimbali kwenye mtandao wa internet.

Karibu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad