Klabu ya Yanga, imesema mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu unakwenda vizuri.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, imeeleza kuwa vikao na washirika wao ambao ni La Liga na klabu ya Sevilla vimeshaanza kufanyika.
Kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Fredrick Mwakalebela amesema, ''tupo katika muendelezo wa mikutano na semina kuelekea mabadiliko ya Klabu, tayari tumeshafanya vikao vinne na watu wa La Liga na Sevilla''.
Moja ya vikao hivyo ni pamoja na semina ya kushirikiana na wataalamu kutoka La Liga na Sevilla FC kuhusu matumizi ya takwimu kwenye uendeshaji bora wa Klabu.
Mpango huo wa mabadiliko umepangwa kutekelezeka ndani ya miaka mitatu ambapo baada ya muda huo klabu itakuwa imepata mfumo sahihi wa kujiendesha