Mchekeshaji, Idris Sultan, amesema hataki kuwa mnafiki kwani Steven Nyerere alimuongelea maneno mabaya kwenye mahojiano.
Idris amesema hata kama kulikuwa na ukweli au la alipaswa kumuambia moja kwa moja.
“Sitaki kuwa mnafiki, kaka Steve juzi kaniongelea mbovu sana kwenye interview, mambo ambayo hata kama ni kweli au la aliweza kuniambia personally,” aliandika Idris katika ukurasa wake wa Twitter.
“Nikahojiwa na Mimi nikasema siwezi ongea ni mkubwa wangu tena hasa sasa anavyotafuta ugali wa chama. Allah be with you wakati huu mgumu,” alisema.