Kwa kweli hii interview ya Salama na Idris Sultan ni funzo kubwa kwa vijana. Vijana wengi pale wanapopata pesa za ghafla hupata kiwewe na kufanya maamuzi ya kukurupuka na mwisho kujikuta wakianzisha biashara na miradi bubu.
Pamoja na Idris Sultan kuwaomba BBA wasimpatie pesa mapema ili aweze kujitafakari cha kufanya lakini hiyo haikumsaidia. Idris sultan anasema alipopata milioni mia sita baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya BBA alimwamini rafiki yake aitwaye Mike wakaanzisha biashara ya madini.
Idris alimuamini rafiki yake huyo na kumuachia asimamie kila kitu alipokuja kushituka milioni mia sita ilikuwa imekwisha. Kwa mujibu wa idris kitu pekee cha maana alichofanyia zile pesa ni kununua gari la shilingi milioni 30.
Baada ya pesa hizo Kwisha alishindwa kulipa kodi kwenye nyumba za akina Ghalib akarudisha vyombo kwa mama yake mdogo aishiye kimara. Akamfuata Ruge Mutahaba na kumuomba kazi ya utangazaji ili aweze kulipa madeni aliyoyapata kutokana na biashara ya madini. Anasema mshahara ukawa unaenda kulipa madeni yeye akawa anaambulia laki tatu tu kila mwezi.
Baadaye alijipanga na kutafuta wawekezaji akaanza biashara ya viatu akainuka tena mpaka kufikia hatua mwaka 2018 aliingiza milioni mia tatu kwa mwaka.
Hakika vijana tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Idris Sultan na aliyoyapitia.
Msikilize