Ifahamu Safari ya Lissu Kurejea Tanzania
4
July 09, 2020
LICHA ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kutangaza tarehe ya kurudi Bongo, baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa wamesema kuna shaka kama kweli anaweza kurejea nchini.
Wachambuzi hao waliozungumza na gazeti hili jana walisema Chadema awali kilitaka kihakikishiwe na Jeshi la Polisi usalama wa Lissu atakaporejea nchini, jambo ambalo hadi sasa hakuna taarifa za uhakika kuhusu hakikisho hilo.
Hivi karibuni Lissu alisema atarejea nchini kwamba itakuwa Julai 28, 2020 ili ahudhurie vikao vya juu vya chama vitakavyopitisha mgombea wa urais, ubunge na udiwani na yeye amejitokeza kuwania urais kupitia Chadema na kwamba tayari ameshakata tiketi ya ndege kurejea nchini.
Mmoja wa wachambuzi wa kisiasa, Abraham Kassim aliliambia gazeti hili kwamba ana shaka kama Tundu Lissu anaweza kurudi nyumbani kwa sababu amekuwa akisitisha mara kwa mara kurejea nchini kwa sababu alizodai kuwa za usalama wake.
“Mwaka jana Tundu Lissu ambaye alinusurika jaribio la kuuawa miaka mitatu iliyopita, aliwahi kusema mara kadhaa hadharani kwamba hayuko tayari kurudi nyumbani na ataendelea kubakia ughaibuni hadi pale atakapohakikishiwa na Serikali ya Tanzania usalama wake, anadai hajahakikishiwa, atarudije?” alihoji mchambuzi huyo.
“Lissu aliwahi kusema kwamba angerejea nchini Septemba 7 kuadhimisha siku aliyopigwa risasi na kuahidi kuwa angeshiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, lakini hakurudi, vipi leo tuamini kwamba atarudi mwisho wa mwezi huu?” alihoji.
Hata hivyo, baada ya ahadi hizo kutotimizwa na Lissu Chadema kilisema kinaafikiana na uamuzi wake wa kutorejea kikisema kuwa yale yaliyomkumba miaka mitatu iliyopita wakati akireja kwenye maskani yake akitokea katika vikao vya bunge bado ni tishio kwa sababu waliomshambuliwa hawajakamatwa.
Chama hicho kilisema jaribio la Lissu kurejea nyumbani kama alivyokuwa ameahidi hapo awali kuwa angerejea Septemba 7 mwaka jana zoezi lilisitishwa hasa baada ya kujitokeza baadhi ya watu wakimtishia kumdhuru wakati anaporejea nyumbani.
Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema ingawa mwanasiasa huyo haijulikani ni lini atarejea lakini alisisitiza kuwa suala la usalama wake ndiyo linalopewa kipaumbele kwa sasa.
Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro aliwahi kukaririwa akisema kwamba usalama hapa nchini upo na alimtaka Lissu kurejea nchini bila shaka yoyote.
Tundu Lissu aliyevuliwa ubunge mwaka jana na Spika Job Ndugai, amekuwa akiishi nchini Ubelgiji tangu aliponusurika kifo baada ya kushaliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka 2017. Aliwahi kusema ingawa sababu za kiafya za kuendelea kukaa nchini Ubelgiji haziko tena, lakini hakusudii kurejea nyumbani kwa sababu za kiusalama.
STORI | ELVAN STAMBULI, Risasi
Tags
Karibu. Wewe usidanganye Toto.
ReplyDeleteMuhamiaji / Mtafutaji WA Rufugee status.huko Duniani
ENDELEA kutupaka matope na anzisha huko alicho fanya Faru Joni. Nikupe utangulizi WA Filemu yako. NI kama ifutavyo.
1.Nilikuw na Nia ya kurudi Tanz.
2.Nilikuwa.a shaka na Usalama
3.Nimepata Habari M/Kiti hakupenujio wangu na akaniwekea mizengwe Chamani.
4.Dokta wangu amenishauri niendelee na matibabu kwa sasa.
5.Niliomba na kutia Nia mtandaoni LA WaTanzania waliojismatphonisha NI Wachache.
6.TUME HURU YA UCHAGUZI haipo.
7. Demokrasia inaminywa.
8.Wapiga kura wamepeqa Vitisho na ACT zanzibar Kama NI Noma na iwe Noma..
9.Membe na Nyalandu pia Ndani
10. Isitoshe na MwenyeChama pia ndani katika kinyanganyiro??
......N. K
Kwa hiyo sitoweza kurudi kwa Miaka Mitano ijayo.
Awaiting Award at Mlimani city 2030 best script / Best Actor / best character.
Tundu Oyee.. Twita Oyee.. Fesibuku Safiii..!!!!
Lissu lipi kaika hayo ya hapo inadhani na kufikiri labda ungeliweza Kuwafanyia Watanzani.. Sio Mtandaoni. Manayake Magu kafanya kweli na tunaona.
Delete1. Rais Magufuli anatutoa kwenye usafiri wa treni wa enzi za kikoloni unaotumia muda mrefu njiani anatupeleka kwenye ujenzi wa usafiri wa treni wa kisasa kwa standard gauge unaotumia umeme na muda mchache njiani kusafirisha Watu wengi na mizigo mingi. Na Hivi Juzi tumeshuhudia akifungua Handaki la Reli katika Mlima Kilosa... Ni habari nyingine kabisa katika Historia ya Tanzania.
2. Anatutoa kwenye usafiri wa anga wa ndege uliokufa anatupeleka kwenye ufufuo wa shirika la ndege lenye ndege kwa kununua ndege mpya 11 zikiwemo Dreamliner 787-8. na Airbus. na Bombadier
3. Ametutoa kwenye shirika la simu lililokufa ametupeleka kwenye ufufuo wa shirika la simu linaloleta ushindani mkubwa kwenye makampuni ya simu yaliyokuwapo kutokana na ubora wa huduma na wa gharama nafuu. toka 220 mpaka sh 40 tu kwa sasa. nani kama Magufuli ..!!!
4. Ametutoa kwenye uchumi uliokuwa asilimia 5.1 hapo awali mpaka kutupeleka kwenye uchumi unaokuwa wa zaidi ya asilimia 7.2
5. Ametutoa kwenye mzigo wa kulipia elimu mpaka kutupeleka kwenye elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari. Nani kama Magufuli 2020 Hii??
6. Amewatoa akina Mama Wajawazito kwenye mateso ya kujifungulia sakafuni ametupeleka kwenye faraja kwa akina Mama Wajawazito kujifungulia vitandani. Mjamzito mmoja, kitanda kimoja.
7. Ametutoa kwenye mateso ya kulanguliwa dawa na ukosefu wa dawa kwenye hospitali za Serikali ametupeleka kwenye upatikanaji wa madawa mahospitalini uliofikia kiwango cha upatikanaji cha asilimia 92, tena kwa bei nafuu.
8. Ametutoa kwenye usumbufu na mateso kwa Wamachinga na Mama Ntilie kusumbuliwa na Wagambo mpaka kutupeleka kwenye utulivu na amani ya kutosumbuliwa kwa Wamachinga na Mama Ntilie.na Vitambulisho vya Wajasiri Amali kuvitoa kwa elfu 20000 tu. Biashara isiyo zidi mtaji wa millioni Nne.
9. Ametutoa kwenye mfumo wa kuleana na kuchekeana dhidi ya wabadhilifu na wala rushwa na kutupeleka kwenye mfumo wa uwajibikaji wa kupelekwa mahakamani kwa wala rushwa na Mafisadi. na uchumi wetu umepanda kwa kasi na kushika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Karibu. Wewe usidanganye Toto.
ReplyDeleteMuhamiaji / Mtafutaji WA Rufugee status.huko Duniani
ENDELEA kutupaka matope na anzisha huko alicho fanya Faru Joni. Nikupe utangulizi WA Filemu yako. NI kama ifutavyo.
1.Nilikuw na Nia ya kurudi Tanz.
2.Nilikuwa.a shaka na Usalama
3.Nimepata Habari M/Kiti hakupenujio wangu na akaniwekea mizengwe Chamani.
4.Dokta wangu amenishauri niendelee na matibabu kwa sasa.
5.Niliomba na kutia Nia mtandaoni LA WaTanzania waliojismatphonisha NI Wachache.
6.TUME HURU YA UCHAGUZI haipo.
7. Demokrasia inaminywa.
8.Wapiga kura wamepeqa Vitisho na ACT zanzibar Kama NI Noma na iwe Noma..
9.Membe na Nyalandu pia Ndani
10. Isitoshe na MwenyeChama pia ndani katika kinyanganyiro??
......N. K
Kwa hiyo sitoweza kurudi kwa Miaka Mitano ijayo.
Awaiting Award at Mlimani city 2030 best script / Best Actor / best character.
Tundu Oyee.. Twita Oyee.. Fesibuku Safiii..!!!!
10. Ametutoa kwenye mateso ya Wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati na kukosa maabara. Leo hii ametupeleka kwenye hatua ya ukamilifu wa uondoshaji wa tatizo la madawati nchi nzima na maabara kwa baadhi ya shule.
Delete11. Anatutoa kwenye uondoshaji wa tatizo la foleni jijini Dar na kutupeleka kwenye ujenzi wa barabara za juu (flyovers) za Tazara na Ubungo. ambazo Zote zimeshaanza kutumika.na Ubongo inamaliziwa ya Juu kabisa kwenda Sam Nujoma.
12. Amewatoa Wanazuoni wa chuo kikuu cha UDSM kwenye mateso ya kupanga na leo hii amewapeleka kwenye makazi bora ya mabweni ya kisasa wanayolipia gharama za chini kabisa. Mabweni ya Magufuli ambayo pia yalitusaidia katika Janga la CORONA. ambayo mungu katuepusha ... Alhamdullah
13. Ametutoa kwenye balaa la utendaji na uwajibikaji wa hovyo kwa Watumishi Hewa wa umma na ametupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha kuridhisha cha uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma.Na kuwafuta waajiriwa Hewa waliokuwa kila Kona.
14. Ametutoa kwenye utitiri wa kodi kwenye kilimo na Ufugaji na kutupeleka kwenye ufutwaji wa kodi mbalimbali za kilimo na kukifanya kuwa chenye tija kwa Wakulima. Leo hii bei ya korosho imepanda kutoka Tsh. 800 kwa kilo mpaka kufikia Tsh. 2400 kwa kilo.
15. Ametutoa kwenye usiri mkubwa wa mikataba na taarifa za madini na kutupeleka kwenye uwazi taarifa na mikataba ya madini. Leo hii tunajivunia mafanikio ya gawio sawia la faida za madini na Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini. na Faida ni Hamsini kwa Hamsini Barrick na tumeanzisha Twiga ambalo ni Partnership na Barrick ni la KiTanzania na Wazawa wapo Kazini. Si Magumashi kama ACCACIA.
16. Ametutoa kwenye tatizo zito na sugu la ajira na kutupeleka kwenye ongezeko la fursa za ajira kupitia kwenye viwanda zaidi ya 3000, kuwatimua wenye vyeti vyeki, miradi ya ujenzi ya bomba la mafuta, flyovers ya Ubungo na Tazara Mfugale Tunapita na reli ya kisasa ya standard gauge.
17. Ametutoa kwenye makusanyo ya Tsh. Bilioni 800 kwa mwezi mpaka kufikia kwenye makusanyo ya Tsh. Trilioni 1.3 kwa mwezi. Hali hiyo imeimarisha uwezo wa Serikali kibajeti.Na sasa Tanzania tumeingia Uchumi wa Kati.
18. Ametutoa kwenye urasimu na umangimeza kwa viongozi na kutupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa viongozi wa Serikali. Leo hii hakuna usumbufu kumuona kiongozi na viongozi wengi wapo site palipo shida za Wananchi wakizitatua.
19. Ametutoa kwenye mfumo wa walio nacho kujiona Mungu mtu na kuleta ukandamizi ndani ya jamii na kutupelekea kwenye uondoaji wa tabaka la uonevu kwenye masuala ya ardhi na sheria. Lukuvi na Mwigulu wako Kazini. Na Kabudi Nje kaishika Ipasavyo.
20. Ametutoa kwenye mkwamo wa Serikali kuhama Dar es Salaam na kutupeleka kwenye hamisho la Serikali kuhamia Dodoma. Ambao Umekamilika na Yeye na Mama Janeti wako Chamwino Raha mustarehe na Ikulu inajengwa na Wanyama Ndani kama Mbuga.