Nyama ya mbwa yapigwa marufuku katika mkoa wa NagalandKaskazini-Mashariki mwa India.
India yapiga marufuku nyama ya mbwa katika mkoa wa Nagaland , mkoa ambao unapatikana Kaskazini Mashariki mwa India.
Kulingana na taarifa ziliztolewa katika jarida la The Indian Express ni kwamba katibu wa jimbo la Temjen Toy nchini India amesema kwamba serikali imechukuwa uamuzi wa kupiga marufuku biashara ya nyama ya mbwa kwa hali yeyote.
Nyama mbwa ilikuwa ikiliwa kitamaduni katika majimbo ya Kaskazini-Mashariki mwa India.
Baadhi ya mashirika ya kiraia katika maeneo hayo yamekemea uamuzi huo wakati ambapo shirika la kimataifa la haki za wanyama limepongeza uamuzi huo uliochukuliwa na serikali.
Zaidi ya mbwa 30 000 kila mwaka huuzwa katika masoko ya majimbo hayo ambayo yana utamaduni wa kula mbwa Kaskazini-Mashariki mwa India.