Iran Yaiwashia Moto Marekani, Yashambulia Meli yake kwa Mabomu Makali
0
July 29, 2020
Iran imeshambulia kwa makombora makali meli bandia ya kivita ya Marekani katika mlango bahari wa kimkakati wa Hormuz.
Zoezi hilo lilishirikisha mashambulio makali hatua iliofanya kambi mbili za Marekani kujiweka katika hali ya tahadhari.
Jeshi la Marekani lilishutumu tabia hiyo mbaya iliotekelezwa na Iran ikiitaja kama jaribio la kutishia na kichokozi.
Zoezi hilo linajiri wakati ambapo kuna hali ya wasiwasi kati ya Tehran na Washington katika eneo la Ghuba.
CHANZO CHA PICHA,EPA
Maelezo ya picha,Wanajeshi wa Iran walirusha makombora wakilenga meli ya Marekani
Meli hiyo ya kivita inayofanana na ile ya Marekani ambayo mara nyingi hutumiwa kubeba ndege za kivita inaonekana ikiwa imebeba ndege bandia ikiingia katika eneo la Ghuba.
Makombora baadaye yanarushwa kutoka maeneo tofauti ikiwemo mengine ambayo yanailenga meli hiyo.
Kombora jingine ambalo linarushwa kutoka kwa ndege aina ya helikopta linaonekana likipiga upande mmoja wa meli hiyo bandia.
Kile kilichooneshwa katika zoezi hilo yalikuwa mashambulizi kutoka angani na kupitia wanamaji, alisema kamanda wa jeshi la Iran la Revolutionary Guard Jenerali Hossein Salami akizungumza na runinga ya taifa hilo.
Shambulio la kombora la masafa marefu liligunduliwa hatua iliowafanya wanajeshi wa Marekani kuchukua tahadhari katika kambi zao za UAE na Qatar, lilisema jeshi la Marekani.
”Marekani hushirikiana na mataifa mengine kufanya mazoezi ya kukuza usalama wa baharini ili kuunga mkono uhuru wa meli kusafiri, huku Iran ikifanya mazoezi ya kushambulia, ili kujaribu kutishia na kuchokoza”, alisema kamanda Rebecca Rebarich, msemaji wa jeshi la wanamaji wa Marekani akiwa nchini ya Bahrain.
Tags