Jafo Amtimua Meneja wa TARURA Arusha – Video


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo,  amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) Mhandisi Victor Seif kumhamisha mara moja aliyekuwa Meneja wa Tarura Jiji la Arusha na kumpangia kazi nyingine ya kiwango cha chini.

Ametoa maagizo hayo jana wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, mkoani Arusha.

Jafo alisema ameamua kumhamisha mtumishi huyo kutokana na kutotoa taarifa za miradi ya maendeleo yanayofanywa na Serikali, jambo ambalo linasababisha Serikali ionekane inashindwa kutimiza majukumu yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

Amewaagiza watendaji wa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo na kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili wananchi waweze kuijua na kutambua kuwa miradi hiyo imefanywa na Serikali.

“Watendaji wote nchini mna wajibu wa kuhakikisha mnasimamia miradi ya maendeleo kwa weledi mkubwa ili iweze kukamilika kwa wakati na kuitangaza kwa wananchi ili waweze kuijua, kuitunza na kuithamini miradi hiyo,” amesisitiza.

Aidha amewaagiza watendaji wote nchini ambao wamepewa dhamana ya kuwahudumia wananchi watimize majukumu yao kikamilifu ili kutatua kero za wananchi kwa wakati na kuleta maendeleo kwa jamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad