Jinsi Damu Yenye Rangi ya Buluu Kutoka kwa Kaa inavyotumika Kukabiliana na Corona
0
July 09, 2020
Kaa ana macho kumi , amekuwepo kwa takriban miaka milioni 300 na sisi hutumia damu yake ya buluu kuimarisha afya yetu.
Naam sio uongo ni sayansi ya jadi.
Kwa miongo kadhaa tumemuhitaji mnyama huyu wa baharini na damu yake kutenegeneza dawa.
Na wakati huu wa Covid-19 dawa hiyo haijasahaulika, Wanasayansi wanamtumia mnyama huyu kuchunguza uwezekano wa kupata chanjo ya corona.
Kama zamani , wanamazingira walihoji jinsi utafiti wa matibabu unaathiri maisha ya kaa na kutaka wasitolewe damu.
Je wanyama hawa wanatusaidia vipi?
Wanyama hawa wa zamani ni muhimu kwasababu damu yao ya buluu huwasaidia wanasayansi kuhakikisha hakuna viini hatari vya bakteria katika dawa mpya zinazotenegenzwa , bakteria ambao wanaweza hata kuuwa .
Kiwango kidogo cha damu hiyo huviua viini hatari na wanasayansi huitumia kuchunguza iwapo dawa mpya ziko salama. Na ni damu ya kaa hao ambayo sisi wanadamu tumefanikiwa kuipata ili kuweza kufanya hivyo.
Kila mwaka , maelfu ya kaa hukamatwa na kupelekwa katika maabara nchini Marekani ambapo damu yao hutolewa katika mishipa ya damu iliopo karibu na moyo wao.
Baadae huachiliwa na kurudi katika asilia yao.
Hakuna anayejua athari yake .
Awali , wataalam walidhani kwamba kaa wote waliishi baada ya kutolewa damu hiyo.
lakini katika miaka ya hivi karibuni , inakadiriwa kwamba hadi asilimia 30 hufa baada ya shughuli hiyo.
Tags