Wasanii wawili ambao ni mahasimu wakubwa katika game ya muziki wa Bongo, Diamond Platnumz na Alikiba, leo wamekutanishwa na Rais John Magufuli alipowaalika Ikulu ya Chamwino Dodoma, mualiko alioutoa kwa wageni wote walioalikwa kwenye mkutano mkuu wa CCM Dodoma, wasanii wakiwa miongoni mwao.
Akizungumza Ikulu, Rais Magufuli ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha wasanii hao kukutana na kushare jukwaa moja, Alisema ” Unapoona Ali Kiba na Diamond wamekaa pamoja unaona nguvu ya CCM. Unapomuona Harmonize anamsifia Diamond.
Hii ndio Tanzania ninayoitaka” Alisema Rais JPM akionyesha Kuguswa na jinsi wasanii hawa walivyozika tofauti zao, na kuungana pamoja kwa maslahi ya Chama cha Mapinduzi.