Kauli ya Waziri Kigwangala Baada ya Shilole Kupigwa na Mumewe



Kutoka Kwenye Ukurasa Wa Instagram Wa Waziri Wa Utalii Hamisi Kigwangalla Naye Ameonekana Kuguswa Na Suala Lililo Mkuta Mwanamuziki SHILOLE, Waziri Ameandika ..

"Amefanya nini (Shilole) kinachostahili kipigo chote hiki? hivi Mwanaume ukiishampiga hivi Mkeo utaweza kumuambia tena 'nakupenda' ? na kumuita tena 'honey', 'love' lawalawa', nk?, unavyompiga hivi unakuwa umepeleka wapi upendo, huruma, Ubinadamu na Uanaume wako?- Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla @hamisi_kigwangalla

"Hakuna kosa linaloweza kuhalalisha kipigo kwa Mkeo cha namna hii, hakuna, labda kama utuambie kwamba aliyetoa kipigo hiki ana aina moja wapo ya ugonjwa wa akili na amesahau kunywa dawa zake za siku hiyo, si vingine, Wanaume tuna wajibu wa kuwapenda, kuwahurumia na kuwahudumia Wake zetu"- KIGWANGALLA

"Tutimize wajibu wetu huu sio vinginevyo kama unaona Mwanamke amekushinda zungumza kumuacha ama kumrudisha kwao, ama kumruhusu aondoke na si kumpiga" - KIGWANGALLA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad