Kenyatta amesema bendera ya Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti kuanzia Julai 27, 2020 hadi Julai 29, 2020 ikiwa ni sehemu ya kuomboleza kifo hicho na kumuenzi kiongozi huyo wa Tanzania.
“Nawapa pole Watanzania wote na familia ya Mkapa kwa kuondokewa na mpendwa wenu, Mkapa alikuwa kiongozi bora aliyesimama kidete kuiungansha Afrika Mashariki,” amesema Kenyatta.