Kesi ya Mkurugenzi wa Jamii Forums Kutajwa Tena Leo
0
July 30, 2020
Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi wa Jamii Forums na Mwanahisa wa Jamii Media) inatajwa tena leo, Julai 30, 2020 asubuhi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar
Mara ya mwisho iliposikilizwa Juni 25, 2020 Jamhuri iliiomba Mahakama iruhusu kukamatwa kwa Shahidi Tully E. Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma (CRDB) kufuatia kesi hiyo kuahirishwa kwa takriban mara 9
Katika shtaka la kwanza, Mkurugenzi wa Jamii Forums anatuhumiwa kuendesha mtandao (JamiiForums.com) ambao haujasajiliwa Tanzania na vile vile hautumii Kikoa cha do-TZ
Katika shtaka la pili la Shauri hili, Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa Jamii Forums kutoa taarifa kuhusu Wanachama wawili wa Mtandao wa JamiiForums.com waliodaiwa kuandika kuhusu madai ya uhalifu uliokuwa ukiendelea katika Benki ya CRDB
Taarifa zilizotakiwa ni IP-Address, barua pepe, Majina Halisi ya Wanachama hao. Pia ilitakiwa zitolewe post zote zinazohusu Uhalifu unaofanyika CRDB kitu ambacho Polisi wanadai Mkurugenzi huyo aligoma kuwapa
Tags