Kim Kardashian West amezungumzia hadharani matatizo ya afya ya akili ya mume wake Kanye baada ya kuzungumza mara kadhaa mambo ambayo hayakuwa yanatarajiwa siku za hivi karibuni.
Ameanidka kwenye mtandano wa Instagram: "Kama munavyofahamu, Kanye ana tatizo la hisia zinazobadilika badilika.
"Yeyote mwenye tatizo hili au ana mpendwa wake anayepitia hili, anajua vile hili linavyoweza kusumbua na machungu ya kuuelewa."
Ni mtu mwerevu lakini vigumu kumwelewa ambaye wakati mwingine maneno yake hayaendana na nia yake", amesema.
Mwanamuziki huyo ni mmoja wa wanamuziki maarufu Marekani na sasa hivi anajaribu kuwania uraisi wa Marekani. Lakini mkutano wake wa kwanza wa kampeni na ujumbe ambao amekuwa akiandika kwenye mtandao wa Twitter kumesababisha mkanganyiko na wasiwasi.
Kim na Kanye walioana 2014 na kubarikiwa na watoto wanne pamoja.
Katika ujumbe wake Jumatano, Kim ambaye ni mashuhuri katika vipindi vya televisheni na mwanamtindo alisema hajawahi kuzungumza hadharani kuhusu matatizo ya afya ya akili ya mume wake vile yalivyo athiri familia yake "kwasababu ninalinda sana watoto na pia kuna haki ya faragha linapokuja suala la afya yake ".
Ameandika: "Lakini leo, Nahisi nizungumze kitu kwasababu ya unyanyapaa na dhana potofu kuhusu afya ya akili.
"Wale wanaoelewa matatizo ya akili au hata tabia ya kulazimisha wanajua kwamba familia huwa haina la kufanya labda mtu awe hajafikisha umri wa kutambulika kama mtu mzima.
"Watu wasiofahamu au ambao hawajapitia hili wanaweza kuhukumu mtu na wasielewe kwamba watu binafsi lazima wazungumze katika mchakato wa kupata usaidizi hata familia na marafiki wajitahidi kwa kiasi gani."
Kardashian West aliendelea na kusema kwamba mume wake anakosolewa kwasababu yeye ni mtu maarufu na matendo yake wakati mwingine yanaweza kusababisha maoni na hisia kali", lakini akaomba watu kuwa na huruma kupita maelezo na uelewa.
"Ni mwerevu sana lakini ni vigumu kumwelewa ambaye pia ni msanii na mtu mweusi, amepoteza mama yake na anahitajika kukabiliana na shinikizo na kutengwa ambako kumesababisha matatizo ya afya ya akili," aliongeza.
"Walio karibu na Kanye wanajua ni mtu wa aina gani, moyo wake na wanaelewa maneno yake kwamba wakati mwingine huwa hayaendani na nia yake
"Kuishi na matatizo ya afya ya kili hakudidimizi ndoto zake na ubunifu wake.
"Hii ni sehemi ya kipaji chake na kama jinsi ambavyo sote tumeshuhudia ndoto zake nyingi zimetimia.
"Sisi kama jamii tunazungumzia kuhusu upendo katika suala la matatizo ya afya kwa ujumla, hatahivyo, pia tunastahili kuwa na upendo kwa wanaoishi na tatizo hili hasa wakati wanapohitaji hilo zaidi.
"Naomba vyombo vya habari na umma watupe upendo unaohitajika ili tuweze kukabiliana na hili."