Kisa Cha Bi Harusi Aliyefariki Saa chache Baada ya Harusi Yake



Kilikuwa kisa cha kutamausha baada ya habari kuenea kuwa bibi harusi huyo alifariki

Katika baadhi ya picha za harusi mtandaoni, imebainika kuwa mwanadada alitoka hospitalini kufanya harusi hiyo

Mapenzi ni kitu cha ajabu sana na mara nyingi si rahisi kukielewa. Huku wengi wakisema kuwa mapenzi hayana macho, naamini kila anayejihusisha hujihoji kikamilifu kabla kujitumbukiza kwayo.

Naam, mapenzi ya kweli yapo, na iwapo huamini, pia hutaamini kuhusu kisa cha Vivian, bibi harusi raia wa Nigeria aliyefariki siku moja tu baada ya kufunga pingu za maisha.

Vivian na mpenziwe wa dhati walifunga pingu za maisha Jumamosi, Julai 17 kwa harusi ya kukata na shoka na kuonyeshana mapenzi ya kweli bila kujali mapungufu yao.

Harusi yao ilikuwa himizo kwa wengi maana bibi harusi alionekana akiwa mgonjwa na kuwa hata wakati wa harusi, alikuwa ametoka hospitalini kuungana na mumewe katika sherehe hiyo, sindano mkononi ikiwa thibitisho.



Badala ya kutoa gari na mali za dunia, mume huyo alikuwa tayari kutoa maisha yake kwa mkewe aliyekuwa akiugua kumuonyesha mapenzi makuu aliyokuwa nayo kwake.

Harusi ilinoga lakini la kutamausha ni kuwa bibi harusi huyo alifariki  Jumapili, Julai 19, siku moja tu baada ya harusi hiyo.


Hadi sasa haijabainika alichokuwa akiuguza bibi harusi huyo, wengi wakijimwaya mitandaini kutuma jumbe za rambi rambi kwa jamaa na marafiki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad