Korea Kaskazini Yaripoti Kisa cha Kwanza cha Corona


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameitisha kikao cha dharura kufuatia mtu mmoja aliyeshukiwa kuwa na virusi vya COVID-18 kuingia nchini humo kinyume cha sheria.

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali mtu huyo aliingia nchini humo akitokea Korea Kusini na iwapo itathibitishwa kitakuwa ni kisa cha kwanza kutangazwa na serikali ya Korea Kaskazini ambayo imedhibiti maradhi hayo na taifa hilo hadi sasa halikuwa na maambukizi yoyote.


Kulingana na shirika la habari la serikali, KNCA Kim ameitisha kikao hicho cha dharura pamoja na kutangaza kuzuwia watu kubakia majumbani mwao katika mji wa mpakani wa Kaesong. KNCA limearifu kwamba mtu huyo amefanyiwa vipimo kadhaa vilivyotoa majibu yenye utata na hivyo kuwekwa karantini katika mji huo kama hatua ya awali. Hata hivyo haikuwa wazi iwapo alichukuliwa vipimo vya COVID-19.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad