Kutana na Mfalme King Mswati...Ambae Yeye na Mabinti ni Dam Dam...Anawake 15



Ni Mfalme aliyejipatia umaarufu Barani Afrika na duniani kwa ujumla hasa kutokana na utamaduni wake wa kuoa wake wengi.

Mfalme huyo wa taifa la zamani la Swaziland ambalo alilibadilisha jina kulibatiza jina jipya la Ufalme wa eSwatini. Alitoa tamko hilo mwaka jana 2018 wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa alipokuwa akitimiza miaka 50 ya kuzaliwa.

eSwatini, lina maana ya ardhi ya Waswaz na lilitumiwa rasmi na Mfalme Mswati wa tatu kwa miaka mingi. .

Mfalme huyu amejitwalia umaarufu kwa kuoa wake wake 15, ambapo wake zake wawili waliamua kumwacha na wawili wengine walifariki dunia, kwa sasa King Mswati III anadaiwa kuwa na watoto 34 na wajukuu 4.

Katika mila na desturi za Swaziland (eSwatini) Mfalme anahitajika kuchagua miongoni mwa halaiki ya wasichana ‘vipusa’ walio bikra kila mwaka katika ngoma maarufu ya ‘Reed Dance’ inayoitwa Umhlanga. .

Taifa hilo ni mmoja kati ya nchi 16 zilizohudhuria mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad