Aliyekuwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, amehojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kugawa fedha kwa wajumbe wa CCM akiwa nyumbani kwake
Mkuu wa TAKUKURU-Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amesema Lusinde alichukuliwa Julai 7, wakamuhoji kuhusu tuhuma za kuwakusanya wajumbe na kuwapa rushwa ili nao wakawashawishi wengine waweze kumpigia kura katika kura za maoni
TAKUKURU inaendelea na uchunguzi dhidi ya Lusinde kutokana na tuhuma alizokutwa nazo. Kibwengo amesema hawakumshikilia bali walikaa naye kwa saa 4 wakimuhoji na sasa yuko huru huku uchunguzi ukiendelea