Maabara Maarufu Matatani kwa Matokeo Tatanishi ya Covid19
0
July 18, 2020
Maabara ya Lancet imekuwa ikitoa matokeo changanyishi ya covid19
Waziri wa afya Kenya, Mutahi Kagwe alieleza kuwa hatua hiyo imewafanya wananchi kushuku ripoti inayotolewa na serikali kuhusu virusi hivyo
Hii inajiri baada ya ripoti kuhusu watu 18 wa shule mmoja Nakuru waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo kubadilika
Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametaka maabara ya Lancet kufanyiwa uchunguzi kwa kutoa matokeo changanyishi kuhusiana na vipimo vya covid19.
Kagwe alifunguka kuhusu kisa hicho Alhamisi, Julai 16 katika taarifa yake Nakuru siku chache tu baada ya shule ya kibinafsi ya St Andrews Turi kulalamika kuhusu matokeo ya vipimo vya covid19 yaliyopewa wanafunzi wake.
Wanafuzi na walimu 18 walikuwa wameambukizwa virusi vya corona kulingana na vipimo vlivyofanywa na maabara ya Lancet.
Matokeo ya vipimo hivyo vilibadilika baada ya 18 hao kupimwa tena na KEMRI suala ambalo limezua gumzo.
‘ Ni kweli kuwa kuna maabara moja ya Lancet ambayo matokeo yake yalikuwa kando. Ni maabara hayo hayo ambayo yana kisa sawa Nairobi,’’ Kagwe alisema.
‘’ Wizawa itachukua hatua na pia tumeiomba bodi kuchukua hatua. Pia nawaomba msiende katika maabara hayo. Mbona uende katika maabara yatakayokupa matokeo ya kuchanganyisha? Kagwe aliongezea.
Aidha, alisema kuwa maabara kama hayo hayataruhusiwa kuhudumu maana inawafanya wananchi kushuku ripoti ya maambukizi ya covid19 inayotolewa na serikali.
Tags