Maalim Seif : Wapinzai Wanajali Maslahi Yao Binafsi Kuliko Nchi
1
July 04, 2020
Mwanasiasa mkongwe na mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amesema wapinzani wengi nchini wanatazama zaidi maslahi yao binafsi kuliko maslai mapana ya nchi pindi wanapopata nafasi ya uongozi baada ya chaguzi.
Akizungunza wakati wa mahojianao maalum na televisheni mtandao ya Watetezi Tv Maalim Seif amesema kitendo hicho kinatafasiliwa kuwa wapinznai hawako makini na hawana nia thabiti ya kuitoa CCM madarakani.
“Hata mimi niwe mkweli, wapinzani wengi wanajali maslahi yao binafsi, na si maslahi mapama ya nchi. Watu wana sababu kabisa za kutulaumu Upinzani maana tuna ubinafsi, hatupo ‘serious” amesema Maalim
Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi oktoba Tanzania itaingia kwenye uchanguzi mkuu wa wabunge,madiwani na rais, jambo mabalo maalim Seif amewataka wapinzai wanaogombea kuwa na nia thabiti na sio kuweka maslai yao mbele.
Tags
Swadakta Maalim.
ReplyDeleteTena mlafi kweli mpaka Wabunge kawaibia na kajenga hotel Za kitalii Moshi. Sasa Wabunhe wamemfikisha Takukuru. Tamaa Za Maka do kando MBAYA sana