Maamuzi haya ya Uingereza yawakasirisha wasafiri kutoka Hispania



Watalii raia wa Uingereza wanaorudi nchini mwao kutoka Uhispania wamekasirishwa na uamuzi wa ghafla wa serikali yao kuwalazimisha kukaa karantini kwa muda wa siku 14.


Everyone is panicking' over quarantine, says UK tourist in Spain ...


Uamuzi wa Uingereza kuiondoa Uhispania katika orodha ya nchi salama ulitangazwa jana Jumamosi, na kuwaacha njia panda wasafiri wanaoingia Uingereza.


Utawala wa Waziri Mkuu Boris Johnson umekosolewa vikali kwa uamuzi huo ambao umechukuliwa baada ya idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona kupanda nchini Uhispania.


Uhispania ilikuwa kwenye orodha ya nchi salama, hatua hiyo ikimaanisha kuwa sio lazima kwa wasafiri wanaotokea nchini humo na kuingia Uingereza kukaa karantini.

Hata hivyo kufuatia ongezeko la maambukizi ya Covid-19 nchini humo, imelazimu baadhi ya miji kama vile Barcelona kuweka tena sheria za kuwalazimu watu kuvaa barakoa na kuwataka watu kusalia majumbani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad