KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison, leo maamuzi yake yanatarajiwa kutolewa na Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kuhusu suala la mkataba wake ndani ya Yanga.
Jana, Julai Mosi, Morrison aliitwa TFF kuhojiwa ambapo habari zinaeleza kuwa ni kutokana na ishu ya mkataba wake ndani ya Klabu ya Yanga.
Mvutano mkubwa wa Yanga na Morrison ni ishu ya mkataba wake ambapo Morrison anasema kuwa dili lake alisaini la miezi sita na Yanga wanasema kuwa amesaini kwa muda wa miaka miwili.
Pia nyota huyo alisema kuwa amecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara akiwa hajapewa mkataba ndani ya Yanga.
Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa kiungo huyo amethibitisha kuwa alicheza mechi mbili bila kuwa na mkataba.