Magufuli "Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu tulikuwa tunapitia kipindi kigumu cha Corona"


Rais Magufuli amesema kuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo ambayo ameyatenda hasa katika kipindi kigumu cha ugonjwa wa Corona.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati alipounganishwa kuzungumza Mubashara na tamasha la kumshukuru Mungu kwa matendo aliyoyatenda nchini.

“Siku ya leo imenilazimu kuja nikiwa na biblia tunakumbushwa kwenye kitabu cha Yeremea 33:3 ninaomba niusome nisije nikaukosea unasema hivi ” Niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua,”amesema Magufuli.

Aliongezea kuwa ” Sisi Watanzania tumemuita Mungu katika Mambo magumu ambayo tumeamini hatuwezi kuyashinda kwa nguvu zetu. Tumemuita Mungu katika kipindi cha Corona ni kipindi ambacho kilikuwa ni kigumu sana.. Mungu wetu mwema alisikia na akajibu majibu haraka sana,”

Magufuli amesema hata leo wanaposherehekea na kukusanyika kwa wote hakuna mtu ambaye anamuogopa mwenzake kwa sababu ya Corona.

“Shukurani kwa mwenyezi Mungu lakini pia Mungu huyo huyo amejumuika katika mambo mbalimbali ya nchi yetu. Tumeweza kuingia kwenye uchumi wa kati mapema sana kabla ya wakati ilikuwa ni kipindi kigumu katika nchi yetu lakini Mungu ametupigania,” amesema Magufuli.

Rais amesema katika tamasha hilo wamekusanyika watu mbalimbali katika dini lakini wameweza kukusanyika kwa jambo moja.

“Hicho ni kitendo ambacho naona ni cha ajabu kwa Watanzania ninawashukuru sana ndugu zangu viongozi ninawashukuru ninyi nyote mliokusanyika hapa kwa ajili ya jambo hili la kumshukuru Mungu kwa matendo makubwa. Mungu awabariki sana naona kwaya mbalimbali zimependeza kweli nilitamani na Mimi ningekuwa hapo baadaye nikawa namtafuta ndugu Polepole uko wapi angalau ufike tu uniwakilishe.. Asiende kuzungumza ya chama azungumze ya Mungu kwa sababu Mungu ni wa vyama vyote,” amesema Magufuli.

Aidha, Magufuli amesema wanaingia katika kipindi kingine cha uchaguzi ukasimamiwe vizuri na kumtanguliza Mungu uwe wa amani, tupendane na washikamane kwa ajili ya kujenga taifa.

“Mimi ninaamini katika siku zote tukiendelea kumtanguliza Mungu tutashinda. Ninawashukuru sana tumpe Mungu nguvu zake zote wanakwaya, wachungaji, wana Dar es Salaam ninawashukuru sana,” amesema Magufuli.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu Jemedari Ni wa kungwa Mkono Na Wazalendo wote,
    Na inshaallah Kura Zote za Watanzania wenye Akili Timamu Ni Zake.

    Inshallah Tumuombee Mwenyezi Mungu Amlinde na Mahasidi wanapo Husudu na kumjaalia Afya na Siha Njema .. Yaa Rabb...!!


    1. Rais Magufuli anatutoa kwenye usafiri wa treni wa enzi za kikoloni unaotumia muda mrefu njiani anatupeleka kwenye ujenzi wa usafiri wa treni wa kisasa kwa standard gauge unaotumia umeme na muda mchache njiani kusafirisha Watu wengi na mizigo mingi. Na Hivi Juzi tumeshuhudia akifungua Handaki la Reli katika Mlima Kilosa... Ni habari nyingine kabisa katika Historia ya Tanzania.

    2. Anatutoa kwenye usafiri wa anga wa ndege uliokufa anatupeleka kwenye ufufuo wa shirika la ndege lenye ndege kwa kununua ndege mpya 11 zikiwemo Dreamliner 787-8. na Airbus. na Bombadier

    3. Ametutoa kwenye shirika la simu lililokufa ametupeleka kwenye ufufuo wa shirika la simu linaloleta ushindani mkubwa kwenye makampuni ya simu yaliyokuwapo kutokana na ubora wa huduma na wa gharama nafuu. toka 220 mpaka sh 40 tu kwa sasa. nani kama Magufuli ..!!!

    4. Ametutoa kwenye uchumi uliokuwa asilimia 5.1 hapo awali mpaka kutupeleka kwenye uchumi unaokuwa wa zaidi ya asilimia 7.2

    5. Ametutoa kwenye mzigo wa kulipia elimu mpaka kutupeleka kwenye elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari. Nani kama Magufuli 2020 Hii??

    6. Amewatoa akina Mama Wajawazito kwenye mateso ya kujifungulia sakafuni ametupeleka kwenye faraja kwa akina Mama Wajawazito kujifungulia vitandani. Mjamzito mmoja, kitanda kimoja.

    7. Ametutoa kwenye mateso ya kulanguliwa dawa na ukosefu wa dawa kwenye hospitali za Serikali ametupeleka kwenye upatikanaji wa madawa mahospitalini uliofikia kiwango cha upatikanaji cha asilimia 92, tena kwa bei nafuu.

    8. Ametutoa kwenye usumbufu na mateso kwa Wamachinga na Mama Ntilie kusumbuliwa na Wagambo mpaka kutupeleka kwenye utulivu na amani ya kutosumbuliwa kwa Wamachinga na Mama Ntilie.na Vitambulisho vya Wajasiri Amali kuvitoa kwa elfu 20000 tu. Biashara isiyo zidi mtaji wa millioni Nne.

    9. Ametutoa kwenye mfumo wa kuleana na kuchekeana dhidi ya wabadhilifu na wala rushwa na kutupeleka kwenye mfumo wa uwajibikaji wa kupelekwa mahakamani kwa wala rushwa na Mafisadi. na uchumi wetu umepanda kwa kasi na kushika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

    10. Ametutoa kwenye mateso ya Wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati na kukosa maabara. Leo hii ametupeleka kwenye hatua ya ukamilifu wa uondoshaji wa tatizo la madawati nchi nzima na maabara kwa baadhi ya shule.

    11. Anatutoa kwenye uondoshaji wa tatizo la foleni jijini Dar na kutupeleka kwenye ujenzi wa barabara za juu (flyovers) za Tazara na Ubungo. ambazo Zote zimeshaanza kutumika.na Ubongo inamaliziwa ya Juu kabisa kwenda Sam Nujoma.

    12. Amewatoa Wanazuoni wa chuo kikuu cha UDSM kwenye mateso ya kupanga na leo hii amewapeleka kwenye makazi bora ya mabweni ya kisasa wanayolipia gharama za chini kabisa. Mabweni ya Magufuli ambayo pia yalitusaidia katika Janga la CORONA. ambayo mungu katuepusha ... Alhamdullah

    13. Ametutoa kwenye balaa la utendaji na uwajibikaji wa hovyo kwa Watumishi Hewa wa umma na ametupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha kuridhisha cha uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma.Na kuwafuta waajiriwa Hewa waliokuwa kila Kona.

    14. Ametutoa kwenye utitiri wa kodi kwenye kilimo na Ufugaji na kutupeleka kwenye ufutwaji wa kodi mbalimbali za kilimo na kukifanya kuwa chenye tija kwa Wakulima. Leo hii bei ya korosho imepanda kutoka Tsh. 800 kwa kilo mpaka kufikia Tsh. 2400 kwa kilo.

    ReplyDelete
  2. 15. Ametutoa kwenye usiri mkubwa wa mikataba na taarifa za madini na kutupeleka kwenye uwazi taarifa na mikataba ya madini. Leo hii tunajivunia mafanikio ya gawio sawia la faida za madini na Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini. na Faida ni Hamsini kwa Hamsini Barrick na tumeanzisha Twiga ambalo ni Partnership na Barrick ni la KiTanzania na Wazawa wapo Kazini. Si Magumashi kama ACCACIA.

    16. Ametutoa kwenye tatizo zito na sugu la ajira na kutupeleka kwenye ongezeko la fursa za ajira kupitia kwenye viwanda zaidi ya 3000, kuwatimua wenye vyeti vyeki, miradi ya ujenzi ya bomba la mafuta, flyovers ya Ubungo na Tazara Mfugale Tunapita na reli ya kisasa ya standard gauge.

    17. Ametutoa kwenye makusanyo ya Tsh. Bilioni 800 kwa mwezi mpaka kufikia kwenye makusanyo ya Tsh. Trilioni 1.3 kwa mwezi. Hali hiyo imeimarisha uwezo wa Serikali kibajeti.Na sasa Tanzania tumeingia Uchumi wa Kati.

    18. Ametutoa kwenye urasimu na umangimeza kwa viongozi na kutupeleka kwenye uimarishwaji wa kiwango cha nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa viongozi wa Serikali. Leo hii hakuna usumbufu kumuona kiongozi na viongozi wengi wapo site palipo shida za Wananchi wakizitatua.

    19. Ametutoa kwenye mfumo wa walio nacho kujiona Mungu mtu na kuleta ukandamizi ndani ya jamii na kutupelekea kwenye uondoaji wa tabaka la uonevu kwenye masuala ya ardhi na sheria. Lukuvi na Mwigulu wako Kazini. Na Kabudi Nje kaishika Ipasavyo.

    20. Ametutoa kwenye mkwamo wa Serikali kuhama Dar es Salaam na kutupeleka kwenye hamisho la Serikali kuhamia Dodoma. Ambao Umekamilika na Yeye na Mama Janeti wako Chamwino Raha mustarehe na Ikulu inajengwa na Wanyama Ndani kama Mbuga.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad