Mahujaji Wakusanyika Mlima Arafat



Mahujaji wanaotekeleza ibada ya Hija leo wamekusanyika karibu na mji mtakatifu wa Mecca nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kukamilisha ibada hiyo ya kila mwaka, ambayo idadi ya mahujaji imepunguzwa mwaka huu kutokana na janga la virusi vya corona.

Watu elfu kadhaa wanashiriki, ikiwa ni sehemu ndogo ya karibu mahujaji milioni 2.5 ambao kwa kawaida hukusanyika kila mwaka katika mji mtakatifu wa Mecca kwa ajili ya ibada hiyo.

 Mabasi yaliyowabeba mahujaji yalianza kuwasili mapema leo asubuhi katika mlima Arafa, kiasi ya kilometa 20 mashariki mwa Mecca, huku kukiwa na hatua kali za kiafya.

Mlima huo ni mahali ambako mtume Muhammad anaaminika kutoa hotuba yake ya mwisho kiasi ya karne 14 zilizopita.

Mahujaji watabakia katika mlima Arafa kwa siku moja, wakisali na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kuridhika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad