Malawi yaanza siku tatu za maombi dhidi ya Corona






Katika kuendelea kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Serikali ya Malawi imetangaza kuanza kwa siku tatu za kufunga na kumuomba Mungu awaepushe dhidi ya janga la virusi hivyo vinavyoendelea kuisumbua dunia. 

Katika taarifa ya serikali, Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera ametangaza maombi yanaanza leo Julai 16 na yatamalizika Julai 18 mwaka huu na siku inayofuatia, Jumapili Julai 19 wananchi watashiriki kutoa shukrani kwa Mungu kwa mambo aliyolifanyia taifa hilo. 

Kuhusu maombi hayo, Rais Chakwera amewasihi wananchi waombe janga hilo liondoke, Mungu awaponye wagonjwa na awalinde wahudumu wa afya ambao wamekuwa msatari wa mbele pamoja na kuwalinda wale wote ambao hawana maambukizi. 

Chakwera aliapishwa kuwa kiongozi wa taifa hilo Juni 28 mwaka huu kufuatia ushindi alioupata katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Juni 23 baada ya mahakama ya katiba kufuta uchaguzi wa awali uliofanyika Mei 21, 2019 kutokana na kuwa na kasoro mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad