Marekani Yatajwa Kama Taifa Lenye Watu Wengi Masikini zaidi Duniani, Licha ya Kuwa na Mabilione wengi Sababu Zaelezwa


Kinyume na dhana potofu miongoni mwa watu wengi: Marekani, nchi ambayo ni tajiri zaidi duniani, ina viwango vibaya zaidi vya umaskini miongoni mwa nchi zilizoendelea.



Zaidi ya nusu karne baada ya Rais Lyndon B. Johnson kutangaza “vita dhidi ya umasikini,” Marekani bado haijaweza kupata jibu ni vipi inaweza kushina vita hiyo.

Tangu kutangazwa kwa azimio hilo mwaka 1964, nchi hii imekua na mafanikio mazuri kama vile kutua mwezini au kuanzisha intaneti, lakini haijaweza kushusha kiwango chake cha umasikini kwa 12% kutoka 19% kilichokuwepo wakati huo.

Hii inamaanisha kuwa Wamarekani milioni 40 wanaishi chini ya mstari rasmi wa umaskini.

Tatizo lilianza zamani kabla ya janga la hivi sasa la virusi vya corona.

Na ukweli ni kwamba, licha ya kuwa taifa ambalo ndilo lililoathiriwa zaidi na covid-19 na kurekodi viwango vya juu zaidi vya ukosefu wa ajira mwaka huu, tangu msukosuko wa uchumi ulioikumba nchi hiyo mwaka 1930, Marekani kwa sasa imeweza kuepuka kuongezeka kwa umasikini kutokana na mpango serikali kutoa ruzuku, kulingana na utafiti.

Hata kabla ya mzozo wa corona, nchi ilitenga mabilioni ya dola kila mwaka kwa ajili ya mipango ya kukabiliana na umasikini, zaidi ya pato la ndani ya nchi la baadhi ya mataifa ya Amerika Kusini.

Swali ni je ni kwanini umasikini huu unatokea kwa nchi yenye nguvu zaidi duniani?

” Kufeli kwa watu binafsi”
Kuna sababu mbili muhimu za umasikini nchini Marekani, kwa mujibu wa watafiti, moja inahusiana na njia za kutatua tatizo. Nyingine na unafuu.

Kwanza Marekani inakosa mfumo wa thabiti wa usalama wa pato la jamii kuweza kusaidia nchi, kwa mfano marupurupu ya malezi ya watoto sawa na nchi nyingine zilizoendelea.

Nchini Marekani watu milioni 40 wanaishi chini ya mstari rasmi wa umaskini
Nchini Marekani watu milioni 40 wanaishi chini ya mstari rasmi wa umasikini
Mipango ya kuboresha maisha ya jamii ambayo Marekani imeitekeleza katika miongo ya hivi karibuni, kama vile utoaji wa chakula au bima kwa watu wasio na ajira, imeiwezesha kupunguza kiwango chake cha umasikini kwa kiwango fulani, lakini inachukuliwa kama mipango ambayo haiwezi kuendelea kwa muda mrefu.

Sababu za kifikra mara nyingi ndizo zinazochangia:

” Tunauona umasikini nchini Marekani kama kufeli kwa mtu binafsi, hivyo ndivyo ilivyo, watu hawataki kufanya kazi vya kutosha, wanachukua maamuzi mabaya, hawana ujuzi wa kutosha na mambo kama hayo. Kwahiyo ni shauri yako ukiwa maskini. ” anasema Mark Rank, profesa katika Chuo Kikuu cha Washington katika St. Louis, ambaye anafahamika kama mmoja wa wataalamu wakubwa wa kupambana na masuala ya umaskini nchini Marekani BBC.

” Matokeo ni kwamba hatufanyi juhudi za kutosha kusema kweli katika kuandaa sera ya jamii ili kuwainua watu kutoka umasikini,” aliongeza.

Pia alisema kuwa hii inatokana na tofauti za kijamii na ubaguzi wa rangi: jamii za walio wachache hapa huumia kuliko jamii za walio wengi.

Wamarekani wenye weusi kwa ujumla ndio maskini zaidi
Wamarekani wenye weusi kwa ujumla ndio maskini zaidi
Huku asilimia 11 ya watoto wa wazungu nchini Marekani wanaishi katika umasikini, viwango vya umasikini vinafikia asilimia 32 miongoni mwa watoto weusi na aslimia 26 kwa watoto wenye asili ya Walatino, kituo kinachohesabu data kuhusu watoto kilinukuu takwimu zilizokusanywa katika sensa.

“Umaikini mara nyingi huonekana kama tatizo kwa wasio wazungu, na hilo pia hupunguza utashi wa kuwasaidia watu wengine,” anasema Profesa Rank.

“Tafiti zinazoonesha kwamba katika nchi ambazo zina jamii tofauti za watu wenye rangi tofauti, zinakua na uwezekano mkubwa zaidi wa watu wake kuwa na usalama wa kipato chao cha maisha, kwasababu watu huwaona wengine kuwa katika kiwango sawa na chao na wanakua na uwezekano mkubwa wa kujitolea kusaidia watu wengine ,” aliongeza.

Ukosefu mkubwa wa usawa
Kwa upande mwingine, wataalamu wametaja suala la uchumi: Kudhoofika kwa soko la la ajira, ambapo jumla ya asilimia 40 hawana ajira na wamekosa mapato yao katika miongo ya hivi karibuni.

Hii inatokana na sababu nyingi, ikiwa ni pamoja na kutoendelezwa kwa viwanda, kudhoofika kwa muungano ya vyama vya wafanyakazi na mabadiliko ya kiteknolojia.

Wale wanaolipwa mshahara wa chini nchini Marekani wamekua wakikabiliwa na matatizo katika miongo ya hivi karibuni
Wale wanaolipwa mshahara wa chini nchini Marekani wamekua wakikabiliwa na matatizo katika miongo ya hivi karibuni
Kutokuwepo na usawa wa mapato baina ya watu nchini Marekani kunaongezeka nchini Marekani na tatizo hili ni la kiwango cha juu zaidi ya karibu nchi nyingine yoyote iliyoendelea, kwa mujibu wa baraza la mahusiano ya mataifa ya kigeni, kituo kilichopo mjini Washington.

Mratibu wa kituo cha umasikini na sera ya jamii katika Chuo kikuu cha Columbia anasema kuwa nchini Marekani “fursa katika soko la ajira huwa linatolewa mara nyingi kwa watu wenye shahada ya chuo kikuu na wamenufaika na ukuaji wa uchumi .”

” Na sehemu kubwa ya ukuaji wa uchumi haijagawanywa kulingana na mapato wala elimu ,” Wimer aliiambia BBC.

“Chaguo la kisiasa”
Marekani imepata mafanikio ya kijamii katika miongo ya hivi karibuni, kama vile viwango vya juu vya watu waliopata elimu na ujuzi kwa wafanyakazi wake kwa ujumla, na kushuka kwa viwango vya vifo vya watoto wachanga.

Zaidi ya hayo, wataalamu wanaonya kwamba viwango rasmi cha umasikini nchini Marekani vinatolewa kwa kuzingatia mapato ya pesa, havizingatii msaada wa serikali kama vile mikopo, msaada wa chakula wala usaidizi wa nyumba kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini.

Sekta ya fedha ni moja ya sekta zilizonufaika na ukuaji wa uchumi nchini Marekani katika miongo ya hivi karibuni
Sekta ya fedha ni moja ya sekta zilizonufaika na ukuaji wa uchumi nchini Marekani katika miongo ya hivi karibuni
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Wimer na watafiti wengine kutoka mradi wa Columbia unaonesha kwamba, bila kuidhinishwa kwa msaada wa dharura wa janga la virusi vya corona, kiwango cha umasikini nchini Marekani kingepanda hadi kutoka asilimia 12.5 kabla ya janga na kufikia asilimia 16.3.

Lakini marupurupu hayo, ambayo yanajumuisha utoaji wa hundi ya dola 600 zinazotolewa kila wiki kwa mamilioni ya wafanyakazi walioathiriwa na janga la virusi vya corona yanatarajiwa kukoma mwishoni mwa mwezi. Na kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoambukizwa Covid-19, kuendelea kwa mpango huo kutategemea makubaliano baina ya bunge la congress na White House .

Kutokana na janga la corona wataalamu mbalimbali walionya kuwa Marekani haina budi kukubali kuwa ina viwango vya hali ya juu ya umasikini.

“Marekani ni mojawapo ya nchi tajiri zaidi duniani, yenye nguvu zaidi na yenye ubunifu mkubwa wa kiteknolojia; lakini si utajiri wake, mamlaka yake wala teknolojia yake hakuna kinachotumiwa kutoa suluhu ya kukomesha imiongoni mwa raia wake milioni 40 wanaoendelea kuishi maisha ya umasikini” , ilieleza ripoti ya mwaka 2017 ya Philip Aston mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na vita vya umasikini.

Licha ya kuwa na ajira, baadhi ya familia zinashindwa hata kupata chakula
Licha ya kuwa na ajira, baadhi ya familia zinashindwa hata kupata chakula
Alston alieleza miongoni mwa mambo mengine kwamba Marekani ina viwango vya juu vya vifo vya watoto wachanga katika nchi zilizoendelea duniani, viwango vya kuishi vya raia wake vilikua vya chini na viwango vya afya za Wamarekani vilikua ni vya chini zaidi ya nchi nyingine tajiri duniani.

Mkurugenzi wa suluhu za umasikini katika Chuo Kikuu cha Luke Michigan nchini humo, Shaefer, anasema sera rahisi nchini Marekani zinaweza kuwa na ufanisi zaidi katika kupambana na umasikini.

Wataalamu wanaamini kwamba nyingi kati ya raslimali ambazo Marekani inawekeza katika umaskini haziwafikii wanaozihitaji zaidi
Wataalamu wanaamini kwamba nyingi kati ya raslimali ambazo Marekani inawekeza katika umaskini haziwafikii wanaozihitaji zaidi
Utafiti alioufanya na wataalamu wengine wa chuo cha Michigan unaonesha kuwa Marekani huwekeza dola bilioni 278 kila mwaka katika mipango ya kupambana na umasikini , kando na gharama za afya.

Ukiongeza mipango ya huduma za afya kwa ajili ya masikini kama vile Midicaid, uwekezaji huo unafikia hadi dola milioni 857,000, kiwango hicho ni sawa na pato la ndani ya nchi (GDP) la mataifa kama vile Argentina na Chile pamoja.

“Nyingi kati ya pesa hizi haziwafikii masikini zaidi kusema ukweli ,” anasema Shaefer.

Uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba huenda ukatoa fursa mpya kwa Marekani ya kufikiria upya jinsi ya kuboresha matumizi yake.

” Kuna watu kulia na kushoto wanaosema kwamba utendaji huu hautusaidii sisi, tunapaswa kufanya vitu vingine tofauti, tunahitaji kurahisisha mambo, ” anasema

” Nina matumaini kwamba tunaweza kupiga hatua .”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad