Marekani Yatoa ilani ya Vikwazo vya Umoja wa Mataifa Dhidi ya Iran
0
July 31, 2020
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema nchi yake italazimisha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran ikiwa muda wa vikwazo vya silaha vya hapo awali utamalizika.
Urusi na China zenye kura ya turufu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zinataka Iran iuziwe silaha za kawaida baada ya muda wa vikwazo hivyo kumalizika mwezi Oktoba. Vikwazo hiyvo viliwekwa kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka wa 2015.
Waziri Pompeo ameiambia kamati ya mambo ya nje ya baraza la seneti la Marekani kwamba nchi hiyo itapendekeza azimio la kurefusha muda wa vikwazo hivyo vya sasa. Waziri huyo ametamka kwamba ikiwa azimio hilo halitapitishwa, Marekani itachukua hatua za lazima kuhakikisha kwamba Iran inaendelea kuwekewa vikwazo.
Hata hivyo wanachama wengine wa kudumu kwenye Baraza la Usalama Uingereza na Ufaransa wamesema suala la kipaumbele ni kutafuta suluhisho la kidiplomasia ili kukomesha mpango wa nyuklia wa Iran, ingawa pia zinaunga mkono vikwazo dhidi ya Iran.
Tags