Web

Mawaziri 2 wa Afrika Kusini Walioambukizwa Covid-19 Walazwa Hospitalini


Mawaziri wawili wa Afrika Kusini wamelazwa hospitalini siku chache baada ya kubainika kuwa wameambukizwa ugonjwa wa Covid-19 (corona).
Habari hizo zilithibitishwa jana Jumanne na Ofisi ya Rais wa nchi hiyo, ambayo imesema katika taarifa kuwa, wawili hao waliokumbwa na Covid-19 ni Waziri wa Ajira na Leba, Thembelani Nxesi, na  mwenzake wa Madini, Gwede Mantashe.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wawili hao walipelekwa hospitalini siku ya Jumatatu kwa ajili ya matibabu zaidi. Inaarifiwa kuwa, mawaziri hao walikuwa wamejitenga nyumbani, baada ya kugundulika kuwa wameambukizwa maradhi hayo ya kuambukiza karibu wki moja iliyopita.
Hii ni katika hali ambayo, Afrika Kusini inaonekana kuwa kitovu cha maambukizi ya virusi vya corona barani Afrika kwa sasa, ambapo kufikia jana Jumanne, idadi ya visa vya ugonjwa huo vilivyosajiliwa nchini humo ni 372,628, na ile ya waliopoteza maisha kwa maradhi hayo ikiwa ni 5,173.


Kwa mujibu wa Zweli Mkhize, Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, kiwango cha wanaopona ugonjwa huo nchini humo kwa wastani ni asilimia 50 ya kesi zote, na kwamba hadi sasa wagonjwa 195,000 wa corona wamepata afueni.
Idadi ya wagonjwa wa Covid-19 waliothibitishwa hadi kufikia sasa barani Afrika ni zaidi ya laki saba. Hayo ni kwa mujibu wa Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa Afrika (CDC).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad