Mbwa wa kuranda randa mitaani nchini Msumbiji wamekua wakifukua makumi ya makaburi ya watoto katika maziko ya mji wa Chimoio, wakaazi wameambia kituo cha runinga cha Miramar.
Mama mmoja amesema siku chache zilizopita baada ya kumzika mwanawe ,alienda makaburini kufanya usafi lakini alipofika hapo alipata mbwa tayari wamefukua na kula maiti ya marehemu mwanawe.
Ripoti za vyombo vya habari nchi humo zinaonesha vipande vya nguo na , mifupa na nyama ya binadamu iliotapakaa katika eneo la makaburi ya umma.
Mwandishi wa kituo cha runinga cha Miramar ameiambia BBC kwamba katika kipindi cha wiki tatu makaburi 343 ya watoto yalifukuliwa na mbwa.
Wakaazi wanasema mbwa hao wamekuwa tatizo la la kila siku na kwamba hali imekuwa mbaya zaidi katika miezi ya hivi karibuni kwa sababu ni watu wachache wanaoruhusiwa kufika katika maziko hayo kutokana na mlipuko wa virusi vya corona
Janga la virusi vya corona pia limewafanya watu kupoteza kazi na huenda hawana uwezo wa kukimu familia zao wala kuwalisha wanyama wao.
Hatua ya makaburi ya umma kutozungushiwa au imesemekana kuchangia tatizo hilo wenyeji wanasema
Mamlaka ya mji wa Chimoio, ambao ni makao makuu ya mkoa wa Manica karibu na mpaka wa Zimbabwe, haikuwepo kutoa tamko kuhusiana na hali hiyo.